UN yaunga mkono Mkataba wa Hodeida (UNMHA)
Vikosi vya Umoja wa Mataifa pamoja na vikosi vya ulinzi wa pwani nchini Yemeni vimeanza doria rasmi ya maeneo ya bandari katika mji wa Hudayidah nchini Yemeni kufuatilia makubaliano kati ya majeshi ya Houthi yaliyo chini ya uongozi Ansar Allahna na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa Hodeida (UNMHA).
Hakikisho rasmi llimetolewa naUmoja wa Mataifa kuhusu makubaliano hayo yatakayoanza tarehe 14 mwezi mei na mkataba huo utajikita na uondoaji wa vikosi vya kijeshi na uteguzi wa mambomu ya ardhini katika bandari tatu na katika mji wa Hodeida
Luteni Mkuu Michael Lollesgaard amabye ni mwenyekiti wa Kamati ya ushauri wa zoezi la uondoaji wa majesji ya Houthi anasisitiza kuwa hatua hii ni sehemu ya kwanza ya makubaliano ya awali ya uondoaji bikosi kaika mji Hodeida, kwa mujibu wa Mkataba wa Stockholm.
Serikali ya Yemeni imeihakikisha Umoja wa Mataifa kwamba ipo tayari kuwajibika kwa sehemu yake katika awamu ya kwanza pindi itakapoombwa kufanya hivyo. Majadiliano kati ya pande zote katika mgogoro huo nchini Yemeni yanaendelea.