Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kushikilia na kuua watu bila sababu Myanmar ni kinyume cha sheria:UN

Makazi ya wakazi wa kata ya Aung Mingalar mji wa Sittwe, jimbo la Rakhine, Myanmar.
OCHA/P.Peron
Makazi ya wakazi wa kata ya Aung Mingalar mji wa Sittwe, jimbo la Rakhine, Myanmar.

Kushikilia na kuua watu bila sababu Myanmar ni kinyume cha sheria:UN

Haki za binadamu

Kukamatwa kwa vijana na wanaume wanaokadiriwa kuwa 40 hadi 50 nchini Myarmar ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa dhidi ya mustakabali wao imesema ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa hii leo.

Kwa mujibu wa taaifa ya ofisi hiyo iliyotolewa leo vijana na wanaumme hao wameripotiwa kutiwa nguvuni Aprili 30 na kushikiliwa katika shule ya Kyauk kwenye Kijiji cha Tan, Rathedaung  kwenye jimbo la Kaskazini la Rakhine ambako sita kati ya mahabusu hao waliuawa Mei pili na jeshi la serikali.

Kamanda mkuu wa jeshi la serikali ya Myanmar Tatmadaw, aliarifu Mei pili kwamba , jeshi hilo lilifyatua risasi kwa wavulana na wanaume 275 waliokuwa wakishikiliwa mahabusu kwenye shule hiyo na kuwaua mahabusu sita na kuwajeruhi wengine wananane.

Kwa kujibu wa jeshi hilo Tatmadaw , askari walifyatua risasi wakati kundi hilo la wavulana na wanaume walipotaka kuwapokonya silaha , lakini duru zingine zimekanusha madai hayo na kusema Tatmadaw walifyatua risasi bila kubagua baada ya mmoja wa mahabusu kujaribu kutoroka.

Mtoto akiwa katika makazi katika kambi ya Kyein Ni Pyin jimbo la Rakhine, Myanmar.
UNICEF/Ruslana Sirman
Mtoto akiwa katika makazi katika kambi ya Kyein Ni Pyin jimbo la Rakhine, Myanmar.

Jeshi hilo la Myanmar limesema limeanzisha uchunguzi wa tukio hilo. Baada ya kupigwa risasi maiti za wanaume hao sita zililazwa hadharani kijijini kwa ajili ya utambuzi huku zikiwa chini uya ulinzi mkali wa askari ambao jana wameelezewa kuishiwa chakula.

Wanaume na wavulana hao inaaminika walitiwa mbaroni kufuatia mashambulizi mawili kwenye makao makuu ya jeshi la Tatmadaw yaliyofanywa Aprili 9 na kundi lenye silaha linalojiita jeshi la Arakan.

Kutokana na taarifa zilizowasilishwa kwenye ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa jeshi la Tatmadaw lilizingira Kijiji cha Kyauk Tan tarehe 30 Aprili na kuwataka wanaume wote wenye umri wa miaka 15 na zaidi kukusanyika shuleni na wale waliokuwa na umri wa miaka 60 na kuendelea waliachiwa, huku waliosalia wakiripotiwa kunyanyaswa na kuswekwa rumande. Mates ohayo ni pamoja na kunyimwa usingizi na chakula.

Tangu Mei pili wanaume na wavula wengi wamekuwa wakiachiliwa kwa mafungu baada ya kuhojiwa. Hata hivyo hadi wanaume na wavulana 50 bado wanashikiliwa mahabusu bila fursa ya kuwa na mawakili, madaktari au ulinzi wa aina yoyote na wanategemea ndugu zao kwa ajili ya chakula.

Mtoto akiwa anafanyakzi katika ujenzi wa mfereji wa kunyunyuzia maji, Myanmar
ILO/Marcel Crozet
Mtoto akiwa anafanyakzi katika ujenzi wa mfereji wa kunyunyuzia maji, Myanmar

OHCHR inasema hali hii inawatia hofu kubwa na hasa matumizi ya nguvu kupita kiasi, unyanyasaji, kuwaweka rumande, mateso, matumizi ya shule kwa shughuli za kijeshi na kile kinachoonekana ni adhabu ya umati wa watu katika vijiji kutokana na machafuko na vitendo vya kikatili vilivyofanywa na makundi ya watu wenye silaha.

Ofisi hiyo pia imesema inatiwa wasiwasi na tangazo kwamba kisa hicho kitachunguzwa na jeshi, kwani mara kadhaa imeshuhudia chunguzi zinazofanywa na Tatmadaw halizai matunda yoyote kwa waliodhulumiwa.

Hivyo imetoa wito wa kufanyika uchunguzi huru, wa kuaminika na usio na upendeleo. Machafuko na ugomvi kati ya Tatmadaw na jeshi la Arakan umeshika kasi hivi karibuni katika jimbo la Rakhine na ofisi ya haki za binadamu imeitaka serikali ya Myanmar kuheshimu sharia za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu. 

Pia wameitaka serikali kutoa fursa ya kufikia maeneo yote yenye machafuko ikiwemo jimbo la Rakhine ambako vikwazo wa masuala ya kibinadamu vimeongeza madhila kwa wananchi.