Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali za barabarani zazuia manusura kuendelea na harakati zao, Tanzania yachukua hatua

Usafiri wa pikipiki uitwao bodaboda maarufu kama 'mshikaki'
Benki ya Dunia/Stephan Gladieu
Usafiri wa pikipiki uitwao bodaboda maarufu kama 'mshikaki'

Ajali za barabarani zazuia manusura kuendelea na harakati zao, Tanzania yachukua hatua

Masuala ya UM

Wiki ya usalama barabarani ikifikia  ukingoni, tunamulika harakati za kuhakikisha kuna usalama kwa siyo tu waenda kwa miguu bali pia abiria, tunaanzia Uganda na tunamalizia Tanzania. 

Ni Jarida la Ijumaa likiwa na mada kwa kina leo tunaangazia usalama wa barabarani katika kutamatisha wiki ya usalama wa barabarani.

Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO licha ya hatua kubwa zilizopigwa vifo vitokanavyo na ajali za barabarani vinaendelea kuongezeka na sasa kufikia vifo milioni 1.35 kwa mwaka, huku majeraha ya ajali hizo ndio chanzo kikuu cha vifo vya watoto na vijana wa umri wa miaka 5-29.

Mathalani kijana huyu anayezungumza hapa na John Kibego huko nchini Uganda, hawezi kujipatia tena kipato kutokana na kazi yake ya ufundi mchundo anaanza kwa kueleza ajali ilivyotokea…