Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji, unyanyasaji na vitisho dhidi ya watetezi wa haki Colombia vyatutia hofu:OHCHR

Mchoro kwenye moja ya kuta nchini Colombia
UN Mission in Colombia/Bibiana Moreno
Mchoro kwenye moja ya kuta nchini Colombia

Mauaji, unyanyasaji na vitisho dhidi ya watetezi wa haki Colombia vyatutia hofu:OHCHR

Haki za binadamu

Ongezeko la idadi ya watetetezi wa haki za binadamu wanaouawa, kunyanyaswa na kutishwa nchini Colombia ni hali inayotutia hofu kubwa , imesema leo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi.

Ofisi hiyo imesma na hali inazidi kuwa mbaya zaidi na sasa imetoa wito kwa mamlaka nchini Colombia kufanya juhudi kubwa ili kupambana na mwenendo huu wa unyanyasaji na mashambulizi yanayowalenga wawakilishi wa asasi za kiraia na kuchukua hatua zote za lazima kukabiliana na hali ya ukwepaji sheria katika kesi zinazohusiana na hulka hiyo.

Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi hiyo ya haki za binadamu Rupert Colville “Katika kipindi cha miezi minne tu ya mwaka huu jumla ya mauaji 51 ya watetezi wa haki za binadamu na wanaharakati  yameripotiwa na asasi za kiraia, taasisi za serikali na taasisi ya kitaifa ya haki za binadamu.”

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini Colombia inafuatilia kwa karibu madai hayo na kusema idadi hiyo kubwa inaendelea kuonyesha mwenendo mbaya ambao ulishika kasi mwaka 2018 wakati ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilipoorodhesha mauaji ya watu 115 watetezi wa haki za binadamu.

Idadi kubwa ya watetezi wa haki za binadamu wanalengwa nchini Colombia hususani wale wanaoishi maeneo ya vijijini
PICHA/UN Colombia
Idadi kubwa ya watetezi wa haki za binadamu wanalengwa nchini Colombia hususani wale wanaoishi maeneo ya vijijini

Waathirika wakubwa

Ofisi ya haki za binadamu inasema ukiukwaji huo unafanyika kutokana na kuwanyanyapaa watetezi wa haki za binadamu hasa wale wanaoishi vijijini katika maeneo ambayo yanaelezewa kutoka huduma za msingi za kijamii, kuwa na kiwango kikubwa cha umasikini, kwenye kilimo haramu,kughubikwa na makundi haramu na makundi ya wahalifu.

Hivyo ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imesisitiza khaja ya haraka ya “kushughulikia tofauti zilizopo katika kufurahia haki za binadamu hususani za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni hususan kwenye maeneo ya vijijini."

Taarifa hii inasema idadi kuwa na watetezi wa haki za binadamu wanalengwa wakiwemo viongozi wa kijamii, Wacolombia wenye asili ya Afrika, watu wa asili, wanamazingira, wakulima, waandishi wa habari, jamii ya watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja LGBTI, na wanawake watetezi wa haki za binadamu ambao baadhi yao wanajihusisha na masuala ya siasa katika jamii zao.

OHCHR imeongeza kuwa viongozi wa kijamii ndio walio hatarini zaidi kwani zaidi ya asilimia 70 ya walioorodheshwa kuuawa ni wao.

Hofu ya OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema wasiwasi wao mkubwa hivi sasa ni uchaguzi unaotarajiwa mwezi Oktoba kwani idadi ya mashambulizi ya kikatili inaweza kuongezeka zaidi. 

Pia ofisi hiyo imesema inatambua juhudi zilizofanywa na serikali kuboresha ulinzi kwa watetezi wa haki za binadamu na pia katika kuanzisha kundi la majaji waliobobea katika kukabiliana na suala hilo hatua iliyotangwza karibuni na rais Duque.

Pamoja na hatua hizo OHCHR imetoa wito kwa serikali ya Colombia kuongeza mara mbili na kupanua wigo wa juhudi za kuimarisha mazingira ya uhuru na yanayostahili kwa ushiriki wa