Msaada wa haraka wahitajika kwa wakimbizi nchini Sri Lanka baada ya mashambilizi -UNHCR
Msaada wa haraka wahitajika kwa wakimbizi nchini Sri Lanka baada ya mashambilizi -UNHCR
Takribani wiki tatu baada ya kutokea mashambulizi makubwa wakati wa sherehe za pasaka nchini Sri Lanka, shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi kuhusu madhara ambayo mashambulizi hayo yamesababisha kwa wa Sri Lanka wenyewe, na kwa hali inayoendelea kwa maelfu ya wakimbizi na waomba hifadhi waliokimbia makwao baada ya mashmbulizi hayo.
UNHCR inashikiana kwa karibu na serikali, Umoja wa Mataifa na washirika na jamii kuhakikisha kuwa wakimbizi wote na waomba hifadhi wako salama.
Tunaendelea kuwasaidia wale waliohama huku mazungumzo yakiendela na mamlaka kutambua makao mbadala hadi pale wakimbizi watakaparejea makwao. Tumepeleka wafanyakazi zaidi kusaidia serikali, msemaji wa UNHCR Babar Baloch alisema.
Kwa sasa wakimbizi 1,060 na waomba hifadhi, wakiwemo wanawake na watoto wanaishi katika misikiti, vituo vya polisi na vituo vya kijamii wakihofia kuzuka ghasia na vitisho. Wengi waliikimbia nchi zao kufuatia imani zao za dini au siasa.
UNHCR inatoa chakula, madawa na vifaa vya makao hukua ikajaribu kutambua mahitaji zaidi.
Kwa sasa kuna wakimbizi 1,700 waliosajiliwa na waomba hifadhi nchini Sri Lanka. Mamia bado wanaishi kwa amani kwenye vijiji vyao. Sri Lanka imetoa ulinzi kwa miaka mingi kwa wakimbizi kutoka dini na nchi tofauti.