Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR yataka utata unaozunguka kifo cha Alia Abdulnoor kuchunguzwa

Ravina Shamdasani, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.
Photo UN Multimedia
Ravina Shamdasani, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

OHCHR yataka utata unaozunguka kifo cha Alia Abdulnoor kuchunguzwa

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imeitaka Falme ya Nchi za Kiarabu kuchunguza utata unaozunguka kifo cha Alia Abdulnoor. Bi Abdulnoor alifariki katika hospitali ya Al-Ain Mei 4 mwaka huu. Alikuwa akiuagua saratani na anaripotiwa kunyimwa matibabu yanayostahili  na kuzuiwa katika mazingira mabaya.

Wakati ugonjwa ya saratania wa Bi Abdulnoor  wa tangu mwaka 2008  ulijulikana  mwaka 2015, familia yake ilitoa wito wa mara kwa mara kwa mamlaka kumuachilia kwa misingi ya kiafya.

Wito kutoka kwa wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka aachiliwa ili apate kuishi katika mazingira bora wakati wa siku za mwisho mwisho  za maisha yake ulipuuzwa.

Bi Abdulnoor alikamatwa na vikosi vya usalama  Julai mwaka 2015. Aliwekwa katika kizuizi cha siri na kutengwa, ambao alipitia dhuluma za kimwili na kisaikolojia ambapo pia alilazimishwa kukiri makosa baada ya kuteswa.

Bi Abdulnoor alishtakiwa kwa kufadhili ugaidi chini ya sheria zinazopinga ugaidi za mwaka 2014.

Mwezi Februari mwaka 2017 alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.

 “Tunatoa wito kwa mamlaka kuchunguza madai ya kuteswa na kutendewa vibaya Bi Abdulnoor na kuwaleta mbele ya sheria washukiwa wote,” alisema msemaji wa OHCHR Ravina Shamdasani.