Wafanyakazi wenye elimu ndogo wana fursa ndogo sana kuimarisha stadi- Ripoti

6 Mei 2019

Shirika la kazi duniani, ILO na shirika la utafiti la Ulaya, Eurofound yametoa ripoti kuhusu tofauti kati ya viwango vya kazi kote ulimwenguni, ikiwemo idadi ya saa za kazi, tofauti ya malipo kwa misingi ya kijinsia, uwezekano wa hatari za kimwili na fursa za kuimarisha stadi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo imetolewa leo Jumatatu ikilenga wafanyakazi bilioni 1.2, kuna tofauti kubwa katika tofautiza saa za kazi, idadi ya juu ya kazi ngumu na inayomahitaji makubwa na kwamba watu walio na kiwango cha chini cha elimu wanakabiliwa na mazingira mabovu ya kazi na fursa chache za kuimarisha stadi.

Ripoti hiyo ya mazingira ya kazi katika taswira ya kimataifa inatoa taswira ya viwango vya kazi katika mataifa 41 katika kipindi cha miaka mitano ikilenga nchi za Ulaya, China, Jamhuri ya Korea, Uturuki, Marekani nchi za Amerika ya kati, Argentina, Chile na Uruguay.

Utafiti umejikita katika maswala saba ya viwango vya kazi ikiwemo, mazingira, ugumu wa kazi, saa za kazi, mazingira ya kijamii, uimarishaji wa stadi, fursa na malipo.

Matokeo ya utafiti

Tofauti za muda wa kazi ni kubwa miongoni mwa nchi huku mfanyakazi mmoja kati ya sita katika nchi za Ulaya akifanya kazi kwa zaidi ya saa 48 kwa wiki huku jamhuri ya Korea, Uturuki na Chile nusu ya wafanyakazi wakijikuta kaikat hali hiyo. Utafiti umebaini kwamba takriban asilimia 10 ya wafanyakazi hufanya kazi wakati wa muda wao wa mapumziko.

Kazi nyingi na muda mchache na kiwango cha juu cha kazi vinashuhudiwa katika theluthi ya wafanyakazi katika nchi za muungano wa Ulaya na Marekani, Uturuki, El Salvador na Uruguay huku asilimia 25-40 za kazi zikiwa na mahitaji ya kihisia.

Utafiti unaonyesha kwamba watu walio na viwango vidogo vya elimu wanapata fursa chache za kupata nafas iza juu na kuimarisha stadi zao.

Aidha wafanyakazi wengi waliripoti mazingira hatari kwa miili yao, huku utafiti katika nchi zote ukibaini kwamba wanawake hupokea malipo madogo kuliko wanaume na idadi kubwa ya wafanyakazi walio na mishahara midogo ni wanawake.

Takriban asilimia 12 ya wafanyakazi waliripoti unyanyasaji kazini ikiwemo ukatili wa kijinsia na kutukanwa. Kwa mujibu wa ripoti, asilimia 30 ya watu katika nchi zilizoangaziwa wanasewa hawana usalama wa ajira.

Mapendekezo

Ripoti imesisitiza kwamba viwango vya ajira vinaweza kuimarishwa na kupunguza mahitaji kutoka kwa wafanyakazi na kupunguza hatari. Aidha imesisitiza umuhimu wa mazingira rafiki kwa wafanyakazi ikiwamo ambamo wasimamizi na wafanyakazi wenza wanajali, pia majadiliano kwa ajili ya kuimarsha viwango vya kazi.

ILO na Eurofound imetoa wito kwa nchi kote ulimwenguni kuimarisha mazingira ya kazi ikiwemo takwimu juu ya viwango vya kazi, kwa kusema hii ni muhimu kwa ajili ya kutambua masuala yanayozua wasiwasi na kutoa ushahisi kwa ajili ya kuweka sera.

Mwezi uliopita wa Aprili ILO ilitoa ripoti ya mazingira ya kazi na madhara yake kiafya ikisema kila siku watu 7500 hufariki dunia kutokana na mazingira yasiyo salama na afya kazini.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter