Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa ukanda na mkakati mmoja utakuwa chachu ya kutimiza SDGs:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia ufunguzi wa jukwaa la ushirikiano wa kimataifa nchini China.
UN China/Zhao Yun
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia ufunguzi wa jukwaa la ushirikiano wa kimataifa nchini China.

Mpango wa ukanda na mkakati mmoja utakuwa chachu ya kutimiza SDGs:Guterres

Ukuaji wa Kiuchumi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mpango wa Ukanda na mkakati mmoja unaweza kusaidia kupunguza pengo kubwa la fedha ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Akizungumza katika kongamano la kimataifa la “ukanda mmoja, mkakati mmoja wa ushirikiano wa kimataifa “ mjini Beijing China hii leo Gutetrres amesema mpango huo pia unatoa fursa ya hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ameongeza kuwa kufuatia hali ya sasa bila mkakati Madhubuti makubaliano ya kimataifa ya mpango kwa ajili ya watu , amani , dunia na mustakabali bora ambayo ni ajenda ya maendeleo ya mwaka 2030 itafanikiwa nusu utakapofikia ukomo. Kutokana na changamoto kubwa zilizopo iambazo ni pamoja na “mosi rasilimali za kifedha zilizopo kwa nchi zinazoendelea kufikia malengo hayo hazitoshelezi. Pili mabadiliko ya tabianchi yanakwenda kasi kuliko tunavyoyakabili. Ni tatizo kubwa la wakati wet una linaweka hatari kubwa kwa hatma ya nchi zote.”

China ina jukumu kubwa katika ushirikiano wa kimataifa

Guterres ameongeza kuwa na ili kukabiliana na changatomo hii ushirikiano wa kimataifa ni muhimu sana na Uchina ina jukumu kubwa a, akisema uongozi wan chi hiyo katika hatua za mabadiliko ya tabia nchi unasaidia kuonyessha njia.

Akitoa mfano amesema mkakati wa China wa ajira mpya katika sekta ya nishati endelevu hivi sasa imezidi ile ya ajira zinazoundwa katika sekta ya mafuta na gesi na kwamba uwekezaji wa China katika nishati endelevu kwa mwaka 2017 ulizidi dola bilioni 125 ikiwa ni ongezeko la asilimia 25 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Mpango wa ukanda na njia moja kuziba pengo la ufadhili

Katibu Mkuu amesema ifikapo mwaka 2050 angalau asilimia 75 ya miundombinu duniani inahitaji kuwa imejengwa. Dunia inahitaji kushikanmana kutimiza lengo mawili muhimu. “Mosi kufikia kiwango kikubwa cha ukusanyaji rasilimali kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa nchi zinazoendelea duniani na pili kuimarisha uwezo wa kuzuia kasi inayoshindikana na mabadiliko ya tabianchi.” Katika haya amesema mpango wa ukanda na njia moja unaumuhimu mkubwa na wa haraka. Kwa kiwango cha mipango yake ya uwekezaji mpango huo unatoa fursa muhimu ya kuifanya dunia inayojitosheleza na yenye faida kwa wote , na pia kubadili athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.

Katika mustakabali wa dunia

Guterres ametaja kwamba katika kusonga mbele kuna fursa tatu muhimu ambazo zinaweza kunyakuliwa haraka . 

Mosi :

Dunia itafaidika kutokana na mpango wa ukanda na mkakati mmoja ili kusongesha mbele juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu  SDGs. Amesema nguzo tano za mpango huo ambazo ni kuimarisha sera za kuratibu mambo, kuwezesha mawasiliano, biashara, ushirikiano wa masuala ya kifedha na kubadilisha uzoevu wa tamaduni yanauhusiano mkubwa na malengo yote 17 ya maendeleo.

Pili: 

Dunia inahitaji kutumia fursa ya faida itokanayo na mpango huo wa ukanda na mkakati mmoja kusaidia kuziba pengo la ufadhili kwa ajili ya maendeleo endelevu hususani katika nchi zinazoendelea ambako uwekezaji katika miundombinu unahitaji takribani dola trilioni moja.

Tatu: 

Mpango huo wa ukanda na mkakati mmoja unatowa muda wa kuzingatia misingi inayojali mazingira katika miradi mbalimbali. Nchi hivi sasa zinahitaji sio tu barabara na madaraja ya kawaida kuunganisha watu na masoko, lakini pia kutoka kwenye uchumi usiojali mazingira na kuingia kwenye uchumi unaojali mazingira kwa kutumia nishati safi, kupunguza hewa ukaa katika hata ujenzi wa barabara na madaraja siku za usoni.