Kituo cha afya Butembo, DRC chashambuliwa, mfanyakazi wa WHO auawa

19 Aprili 2019

Kwa mara nyingine tena kituo cha afya kimeshambuliwa huko Butembo, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Katika shambulio hilo la leo la kituo hicho kinachotibu Ebola, mfanyakazi mmoja wa shirika la afya ulimwenguni, WHO ameuawa na watu wengine wawili wamejeruhiwa.

Kufuatia taarifa hizo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia za mtumishi huyo wa WHO na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Bwana Guterres ametoa wito kwa mamlaka za DR Congo, zichukue jitihada zote kuwatafuta na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wa shambulio hilo.
 
Katibu Mkuu ameelezea mshikamano wake na wananchi na serikali ya DRC na kusisitiza azma ya mfumo wa Umoja wa Mataifa kuendelea kutokomeza ugonjwa wa Ebola

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter