Ardhi ya kuazima yamwezesha mkimbizi kutoka Sudan Kusini kulea watoto yatima

22 Aprili 2019

Ukarimu wa Uganda wa kuwapatia maeneo ya kilimo wakimbizi kutoka Sudan Kusini, umewezesha wakimbizi kusaidia jamii zinazowazunguka wakiwemo watoto yatima nchini humo.

Nchini Uganda katika makazi  ya wakimbizi ya Oligi, mkimbizi Queen Chandia kutoka Sudan Kusini akiwa kwenye shamba lake la mpunga.

Mgogoro nchini Sudan na Sudan Kusini ambao ulidumu kwa miongo kadhaa ulisababisha maelfu ya watu kukimbia ambapo Queen alikimbilia Uganda katika makazi haya ya wakimbizi akiishi na mama na dada yake.

Mapigano mapya ya hivi karibuni Sudan Kusini yalisababisha maelfu ya wakimbizi kuingia Uganda na ndipo Queen alianza kuchukua watoto yatima na wale ambao walivuka wakiwa hawana waangalizi ili aweze kuwatunza na idadi yao sasa ni 22.

Hata hivyo eneo hili la ardhi alilopatiwa na mwenyeji wake Lagu Samuel limemwezesha kupanda mpunga na kwamba…

(Sauti ya  Queen Chandia)

“Katika kilimo unaweza kuchimba, kupanda mbogambonga na kula, ikimaanisha kuwa ukiwa mtu wa kujitegemea unaweza kufanya kula kitu mwenyewe. Pesa ninayoipta kutoka katika mashamba haya, mosi ninalipa ada ya shule ya watoto wangu na pia ninatumia pesa kupata chakula bora.”

Samuel, ambaye naye aliwahi kuwa mkimbizi anazungumzia kisa cha yeye kumwazima ardhi Queen..ili aweze kulima.

(Sauti ya Lagu Samuel)

“Tulipokuwa Sudan Kusini, ninakumbuka walivyokuwa watu wema kwetu, kwa hivyo nilijisikia kuwa ninatakiwa kuwasaidia hapa Uganda. Na Queen alikuwa mmoja wa wale walioniomba ardhi kiasi nami nikampa kipande cha ardhi li aweze kulima.”

Ardhi ya Samuel inatumiwa pia na mashirika ya maendeleo kuwapa elimu wakimbizi na wananchi wa Uganda kuhusu namna bora ya kulima mpunga.

Minoru Yoshino anafanya kazi na shirika la kimataifa la ushirikiano wa kimandeleo la Japan, JICA.

(Sauti ya  Minoru Yoshino)

“Mpunga ni zao la chakula na biashara. Ulimaji wa mpunga unachangia katika uhakika wao wa chakula na kuboresha ustawi wao.”

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter