Nalaani vikali shambulizi la leo Quetta:Guterres

12 Aprili 2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amesema ameshtushwa sana na shambulio la kigaidi lililotokea mjini Quetta Pakistan. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake mjini New york Marekani, Katibu Mkuu amelaani vikali akiliita shambulio hilo ni kitendo cha kioga na pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha, serikali na watu wa Pakistan huku akiwatakia afuweni ya haraka majerihi.

Kwa mujibu wa duru za habari shambulio hilo la kigaidi limetekelezwa na mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliyelenga soko la wazi kusini Magharibi mwa Pakistan kwenye mji wa Quetta mapema leo Ijumaa na kukatili maisha ya angalau watu 20 na kujeruhi wengine wengi.

Rais wa Pakistan Arif Alvin  waziri mkuu Imran Khan wametoa taarifa za kulaani vikali shambulio hilo na kusema kwamba “halitodhoofisha jitihada za taifa hilo za kupambana na ugaidi.”

Guterres amesema Umoja wa Mataifa unashikamna na serikali ya Pakistan katika vita hivyo dhidi ya ugaidi na ghasia za itikadi Kali.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter