Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan ni lazima mlinde haki na utawala wa sheria-Bachelet

 Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet
ILO/M. Creuset
Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet

Sudan ni lazima mlinde haki na utawala wa sheria-Bachelet

Amani na Usalama

Kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, leo ameukumbusha uongozi wa Sudan kuhusu wajibu wake kimataifa wa kuhakikisha unalinda haki za binadamu kwa watu wote na kujizuia na machafuko.

Kupitia tarifa yake iliyowasilishwa na msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswis mbele ya waandishi wa Habari, Ravina Shamdasani amesema wanafuatilia kwa karibu kinachoendelea na kutoa wito kwa uongozi kujizuia na matumizi ya nguvu dhidi ya wanaoandamabna kwa amani na kuhakikisha kwamba vikosi vya usalama namalaka za mahakama zinachukua hatua kwa kuzingatia utawala wa sheria na wajibu wa kimataifa wa Sudan katika haki za binadamu

(SAUTI YA RAVINA SHAMDASANI)

“Huu ni wakati mgumu na muhimu kwa Sudan, ikighubikwa na hali ya sintofahamu kuhusu mustakabali wake”

Ameongeza kuwa kamishina mkuu ametoa wito wa kudumisha utulivu na kuitaka serikali kuwaachilia watu wote wanaoshikiliwa kwa kutekeleza haki yao ya uhuru wa kukusanyika kwa amani na kujieleza akisema

(SAUTI YA RAVINA SHAMDASANI)

“Inatia moyo kwamba hakukuwa na ghasia usiku wa kuamkia leo ingawa amri ya kutotembea iliyowekwa hapo awali haikuzingatiwa na waliokuwa wakiandamana kwa amani. Pia tumepokea ripoti kwamba kuna baadhi ya mahabusu wa kisiasa ambao wameachaliwa . Hatujaweza kuthibitisha ripoti hizi lakini tunatoa wito kwa mamlaka kuwaachilia mahabusu wote wa kisiasa.”

Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu mgogoro huu nchini Sudan mizizi yake ni malalamiko ya haki za binadamu za kiuchumi, za kijamii, za kiraia na za kisiasa. Na suluhu inapaswa pia kuzingatia haki za binadamu. Pia ofisi hiyo imesisitiza haja ya uchunguzi huru na wa haraka dhidi ya matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.