Skip to main content

Umoja wa Mataifa unafuatilia hali Sudan na kutaka kudumishwa amani na utulivu

Waandamanaji wakiandaman nje ya makao makuu ya vikosi vilivyojihami vya Sudan katika mji mkuu, Khartoum.
UN Sudan/Ayman Suliman
Waandamanaji wakiandaman nje ya makao makuu ya vikosi vilivyojihami vya Sudan katika mji mkuu, Khartoum.

Umoja wa Mataifa unafuatilia hali Sudan na kutaka kudumishwa amani na utulivu

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres anaendelea kufuatilia hali ya Sudan kwa karibu huku akirejelea wito wakudumisha amani na utulivu.

Akihutubia waandishi wa habari mjini New York Marekani msemaji wa katibu mkuu amemnukuu bwana Guterres akikumbusha wito wake na matarajio yake kwamba matakwa ya kidemokrasia ya watu wa Sudan yatafikiwa kupitia mchakato unaofaa , wa kisiasa na jumuishi.

Halikadhalika bwana Guterres amehawkikishia Wasudan utayari wa Umoja wa Mataifa kusaidia nchi hiyo katika siku zijazo.

Duru za kuaminika zinasema serikali ya rais wa Sudan Omar al-Bashir imepinduliwa na kwa sasa inashikiliwa na jeshi.

Omar al-Bashir amekuwa kwenye utawala tangu mwaka 1989 baada ya mapinduzi na kuchaguliwa rasmi rais wa nchi hiyo 1993.

Wataalam walaani matumizi ya nguvu kupindukia dhidi ya waandamanaji

Wakati hali hiyo ikishuhudiwa wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamelaani matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji nchini Sudan. Kwa mujibu wa taarifa yao, wataalma hayo wamesema wamezingatia ripoti za hivi sasa kwamba baraza la kijeshi linaundwa na hivyo kutoa wito kwa mamlaka kushughulikia malalamiko  ya raia.

Kwa mujibu wa wataalam hao zaidi ya watu ishirini wameuwawa na zaidi ya mia moja wamejeruhiwa na kwamba wamepokea ripoti za watu kukamatwa na mashambulio dhidi ya waandishi habari na yanayofanywa na vikosi vya usalama.

“Wakati huu wa mzozo, kuhakikisha uhuru wa haki ya kujieleza, uhuru wa kukusanyika na kulindwa ni muhimu sana,” amesema mtaalum huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kuandamana Clement Nyaletsossi Voule na mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uendelezaji na ulinzi wa haki za kujieleza na kutoa maoni, David Kaye.

Wataalma hawa wametoa wito kwa mamlaka kuhakikisha ulinzi wa raia na wakarti huo wakehimiza jeshi la Sudan na vikosi vya usalama kujizuia kwa ajili ya kuzuia ongezko la vurugu na kuchukua hatua kwa ajili ya kulinda haki za waSudan.

Wakikaribisha mwaliko la serikali ya Sudan kuzuru Sudan kwa ajili ya kutathmini hali Aprili 27 hadi Mei 5, wataalam hao wametoa wito kwa mamlaka kuwezesha uchunguzi wa ukiukaji wa haki za binadamu uliofanyika wakati wa maandamano na kutolea wito vyombo vya kisehrika kusitisha wanachokiita mhakama ya dharura ambazo hazifikii vigezo vya mashtaka yenye haki.

Wataalam hao wa Umoja wa Mataifa wameelezea utayati wao kushirikiana n apande husika kwa ajili ya kuweka mazingira ambapo haki za binadamu zimo kati kati na kwamba sheria inazingatiwa.

Maandamano yalizuka takriban miezi minne iliyopita wakati serikali ilitangaza kuongeza bei ya mkate na bidhaa zingine za msingi.

CERF yatenga dola milioni 26.5 kwa ajili ya Sudan

Wakimbizi wa ndani jimbo la Darfur Sudan wanakabiliwa na changamoto nyingi na ugumu wa kupata maji safi. Pichani ni msichana na kaka yake wakiwa katika kituo cha maji safi cha Abu-Shok kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani illi kuteka maji
UNAMID/Mohamad Mahady
Wakimbizi wa ndani jimbo la Darfur Sudan wanakabiliwa na changamoto nyingi na ugumu wa kupata maji safi. Pichani ni msichana na kaka yake wakiwa katika kituo cha maji safi cha Abu-Shok kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani illi kuteka maji

Wakati huo huo Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock ametangaza kutengwa kwa dola milioni 26.5 kwa ajili ya msaada wa dharura, CERF kwa ajili ya kuwasilisha chakula, lishe, huduma ya afya, maji na huduma ya kujisafi kwa takriban watu 800,000 walioathirika na janga la kiuchumi na chakula linaloshuhudiwa katika majimbo saba Sudan kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.

Bwan Lowcock kupitia taarifa ya OCHA amesema, “janga la kiuchumi linaloshuhudiwa limekuwa na athari zinazokwenda mbali ya uhakika wa chakula. Ongezeko la bei ya chakula inamaanisha kwamba familia zinakulwa chenye upunugfu wa ubora na watoto wengi wachanga na wanawake wajawazito wanaugua. Familia zinakabiliwa na wakati mgumu na wanashindwa kupata tiba, isitoshe kupoteza ajira kunawalazimu kuondoa watoto wao kutoka shule.

Mgao huo wa CERF unalenga wakimbizi wa ndani, wakimbizi na jamii zinazowahifadhi pamoja na wakazi walio hatarini katika maeneo kunakoshuhudiwa ukosefu wa chakula toshelezi ikiwemo, mashariki, kaskazini, kusini na Darfur magharibi, Red Sea, Kordofan magharibi na majimbo ya White Nile.

Ukosefu wa chakula umeongezeka huku ikikadiriwa kwamba watu milioni 5.8 hawana chakula toshelezi tangu Jamuari hadi Machi hii ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishw ana mwaka 2018.

Huduma za ulinzi zitapewa kipaumbele kwa ajili ya mahitaji ya watoto, wanawake na waliohatarini ikiwmo watu wanoishi na ulemavu na walio na magonjwa ya muda mrefu.

Licha ya fecha hizo na zingine kutoka mfuko wa misaada ya kibinadamu ya Sudan dola milioni 21 bado mahitaji ya kifedha hayatoshelezi kufuatia ongezeko la mahitaji. Mwaka huu wa 2019, Umoja wa Mataifa unatarajia kutoa ombi la dola bilioni 1 kwa ajili ya kusaidi watu milioni 4.4 walio hatarini nchini Sudan.