Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yatoa neno baada ya Jeshi la Nigeria kuwahamisha takribani watu 10,000 kutoka katika mji wao wa Jakana usiku wa manane

Mtazamo wa mji wa Rann, jimbo la Borno, Kasakzini-Mashariki mwa Nigeria. Julai 5, 2018
WFP/Inger Marie Vennize
Mtazamo wa mji wa Rann, jimbo la Borno, Kasakzini-Mashariki mwa Nigeria. Julai 5, 2018

OCHA yatoa neno baada ya Jeshi la Nigeria kuwahamisha takribani watu 10,000 kutoka katika mji wao wa Jakana usiku wa manane

Wahamiaji na Wakimbizi

Mratibu wa wa shirika la Umoja wa Mataifa na kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA , Edward Kallon leo ametoa wito kwa serikali ya Nigeria kutoa msaada wa kibinadamu na kuwalinda watoto, wanawake na wanaume takribani 10,000 ambao walilazimishwa kuhamia katika mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri, wakitokea katika mji wao ulioko takribani kilomita 40 kutoka walikohamishiwa.

Ripoti ya OCHA imeeeleza kuwa jioni ya tarehe 8 Aprili 2019 jeshi la Nigeria bila hata taarifa yatahadhari, usiku wa manane liliamrisha  watu takribani 10,000 kuondoka katika mji wa Jakana na likawasafirisha kwa mabasi na Malori hadi kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bakassi. Kwa mujibu wa jeshi hilo, wananchi hao waliahamishwa kwasababu za kiusalama kabla ya operesheni iliyokuwa imepangwa kufanyika katika eneo hilo.

Bwana Kallon amesema,“mji mzima wa Jakana uliachwa mtupu, na watu walilazimishwa kuhamia Maiduguri wakiwa na muda mdogo sana wa kukusanya mali zao. Baadhi ya watu walisema walifika Maiduguri wakiwa hawana chochote, siyo hata viatu miguuni mwao.”

Na hapo ndipo Bwana Kallon akatoa wito, “Umoja wa Mataifa unaisihi serikali kwa haraka kutoa ulinzi, kuhakikisha usalama, kutoa malazi, chakula, maji na huduma za afya kwa raia wasio na makazi na pia taarifa za lini wataruhusiwa kurejea katika makazi yao.”

Umoja wa Mataifa umerejelea ahadi yake ya kusaidia juhudi za kitaifa na za mashinani kuhakikisha kuwa wananchi walioathirika na mgogoro katika maeneo ya Borno, Adamawa na Yobe wanaweza kupata msaada wa kibinadamu na ulinzi wanaouhitaji.

 

TAGS: OCHA, Edward Kallon, Borno, Maiduguri, Nigeria.