Wadau wote tukishikamana twaweza kuwaondolea madhila Wavenezuela:UN

10 Aprili 2019

Hali nchini Venezuela ni teten a mamilioni ya raia wanahitaji msaada wa kibinadamu, lakini kwa mshikamano na msaada zaidi kutoka kwa wadau wote tunaweza kuwapunguzia madhila raia hao.

Hayo yamesemwa na Mark Lowcock mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama hii leo mjini New york Marekani kujadili hali ya kibinadamu nchini Venezuela.

Akieleza hali halisi inayoikabili nchi hiyo Bwana Lowcock amesema kila uchao inazidi kuwa mbaya , bado kuna matatizo ya umeme nchi nzima yanayoathiri mfumo wa afya ikiwemo hospital nyingi kushindwa kutoa huduma za muhimu kama za upasuaji na huduma za dharura, uchumi umeendelea kuporomoka na uwezo wa wananchi wa kawaida kununua bidhaa ukishuka na kuzifanya familia nyingi kushindwa kumudu chakula. Mahitaji ya kibinadamu ni makubwa na yanazidi kuongezeka”.

Katika mkutano huo Lowcock amesisitiza masuala matatu , mosi ni mahitaji ya muhimu na ya haraka ya kibinadamu Venezuela, pili juhudi za kusaidia watu walio katika hali mbaya na wasiojiweza na tatu ni maeneo ambayo yanahitaji msaada wa pamoja.

Mkuu wa masuala ya kibinadamu na shirika la kuratibu misaada ya dharura la Umoja wa Mataifa , OCHA Bwana. Mark Lowcock
UN Photo/Manuel Elias
Mkuu wa masuala ya kibinadamu na shirika la kuratibu misaada ya dharura la Umoja wa Mataifa , OCHA Bwana. Mark Lowcock

Mahitaji ya kibinadamu

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA  takribani watu milioni 7 nchini Venezuela wanahitaji msaada wa kibinadamu ikiwa ni asilimia 25 ya watu wote, na hali ni mbaya zaidi katika majimbo matatu Kusini mwa nchi hiyo,  Zulia na Lara Magharibi mwa nchi. “Watu wenye magonjwa ya muda mrefu, wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, watoto wa chini ya umri wa miaka mitano, watu wanaohama na wanaoishi na ulemavu ni miongoni mwa walio hatarini.”

Lowcock ameongeza kuwa wanakadiria watu milioni 1.9 wanahitaji msaada wa lishe wakiwemo watoto wa chini ya miaka mitano milioni 1.3,  amesisitiza kuwa kupungua kwa huduma za afya kuomeongeza hatari ya vifo vitokanavyo na kisukari, magonjwa ya moyo, saratani na VVU, lakini magonjwa yanayoweza kuzuilika kama kifua kikuu, donda koo surua na malaria vyameibuka upya. Mgogoro huu wa Venezuela pia umeingilia mfumo wa elimu kwa watoto zaidi ya milioni moja na familia nyingi sasa haziwezi tena kumudu mahitaji ya msingi kwa watoto wao kama sare za shule, usafiri na viatu.Pia amesema takribani watu milioni 2.7 wanakadiriwa kuwepo ndani ya Venezuela na wanahitaji msaada wa ulinzi na huduma muhimu.

Wakimbizi kutoka Venezuela wanaolekea nchi jirani mjini  Cúcuta,Colombia wakielekea Pamplona.
© UNHCR/Stephen Ferry
Wakimbizi kutoka Venezuela wanaolekea nchi jirani mjini Cúcuta,Colombia wakielekea Pamplona.

Msaada kwa walio katika hali mbaya

Bwana Lowcock amesema Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu wako Venezuela na wamekuwa wakipanua wigo wa operesheni zao ili kuwafikia wahitaji wengi zaidi na kwa kupitia misaada ya wafadhili na wahisani Umoja wa Mataifa umeweza kutoa kinga na tiba ya utapiamlo kwa watoto 189,000, kuongeza huduma ya afya ya mama na mtoto, umetoa msaada wa genereta 10 kwenye hospital mbalimbali, kuweka matangi ya maji, kutoa dawa za ukimwi na kufikisha chanjo dozi 176,000 kwa watoto.

Jitihada zaidi zinahitajika.

Mratibu huyo amesema licha ya yote yanayofanyika ni dhahiri kwamba jitihada zaidi zinahitajika na kuomba msaada wa Baraza za Usalama kushughulikia mambo matatu. Mosi kuboresha heshima ya misingi ya kibinadamu akisema Venezuela kuna haja ya kutenganisha malengo ya kisiasa na ya kibinadamu na msaada wa kibinadamu ni lazima upelekwe kwa misingi ya mahitaji pekee na si vinginevyo.

Pili mazingira mazuri ya uendeshaji, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa fursa za kuwafikia na watu wenye uhitaji, hatua zaidi zinahitajika katika hilo na tatu fecha zaidi zinahitajika katika kusaidia upanuzi wa mipango ya huduma za kibinadamu kwani fecha zilizopo sasa haziendani na kiwango cha mahitaji

Wakimbizi na wahamiaji wa Venezuela wakivuka daraja la Simon Bolivar nchini Veneuela.
UNHCR/Siegfried Modola
Wakimbizi na wahamiaji wa Venezuela wakivuka daraja la Simon Bolivar nchini Veneuela.

Mgawanyiko katika Baraza la usalama kuhusu Venezuela

Marekani

Makanu wa Rais wa Marekani Mike Pence akishiriki katika mkutano huo kwa niaba ya nchi yake amelitaka baraza la usalama “kutengua hadhi ya serikali ya Nicolás Maduro kwenye Umoja wa Mataifa.”

Pia ametangaza kwamba nchi yake inaandaa azimio la kumtambua Juan Guaidó kama rais wa mpito wa Venezuela. Kwa mujibu wa Pence makundi ya nchi kama G7 na mashirika ya mataifa ya Amerika ymewatambua wawakilishi wa Guaidó kama ni halali nan chi nyingi za Magharibi zinazungumza bayana kwamba ni wakati wa Umoja wa Mataifa kufanya hivyo pia.

Makamu huyo wa Rais wa Marekani ameishutumu serikali hiyo ya Amerika Kusini kwamba inawatia umasikini watu wake na , imewatia jela watu 1255 bila kufuata mchakato halali na kupoteza Maisha ya takriban waandamanaji 40. Ameongeza kuwa “wezi Venezuela hawaibi benki, wala kwenye migahawa ni magenge ya uhalifu ambayo yameigeuza mitaa ya nchi hiyo kuwa uwanja wa vita. Hivi sasa Venezuela amesema ndio yenye idadi kuwa ya mauaji zaidi ya watu 70 kwa siku.”

Ameliita taifa hilo kuwa ni “lililofeli na kwamba kama historia inavyosema taifa lolote lililofeli halitambui mipaka.” Pia bwana Pence amesema “Nicolás Maduro ni dikteta asiye na haki ya utawala halali n ani lazima aondoke.”

 

Venezuela

Samuel Moncada, Mwakilishi wa kudumu wa Venezuela  kwenye Umoja wa Mataifa akihutubia Baraza la Usalama la UN
UN /Manuel Elias
Samuel Moncada, Mwakilishi wa kudumu wa Venezuela kwenye Umoja wa Mataifa akihutubia Baraza la Usalama la UN

Naye mwakilishi wa kudumu wa Venezuela kwenye Umoja wa Mataifa Samuel Moncada amesema hali inayoikabili nchi yake ni matokeo ya “kampeni ya mabavu ya Marekani na Uingereza” akisistiza kwamba “tiba ya hali hiyo hakuwezi kuwa ni dozi mpya ya mabavu ya kuiingilia kupitia mgongo wa masuala ya kibinadamu. Suluhu sio msaada wa wahal;ifu ambao wanataka kujionyesha kama wakombozi, sio katika nji za kibinadamu zilizoandaliwa kuchochea vita, sio katika mikutano ya wafadhili ambayo inaficha uporaji uliofanywa dhidi ya taifa letu.”

Balozi Mocanda ameongeza kuwa “tiba ya hali hiyo ni kurejesha fecha zilizoibwa kwa watu wetu, kwa kusitisha vikwazo vya kibiashara na kifedha kwa taifa letu, kwa kukomesha hujuma dhidi ya miundombinu yetu kwa operesheni zisizofaa  na kusitisha vitisho kwa Wavenezuala ambao wanataka majadiliano, ni lazima tukomeshe vita vya Trump na Baraza la Usalama ni lazima litimize wajibu wake kwa kuihakikishia Venezuela haki yake ya amani.”

Balozi huyo pia ameipinga hotuba ya Pence akisema illisema uongo kwamba shirika la mataifa ya Amerika limemtimua mwakilishi wa Rais Maduro, na kwamba uamuzi ambao ulichukuliwa mbali ya mwakilishi huyo ni jkumjumuisha mjumbe mmoja wa baraza la taifa linaloongozwa na Juan Guaidó.

 

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter