Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajisikiaje kusubiri kunyongwa kwa kosa ambalo hukufanya?

Si haki mtu kukaa gerezani kwa muda mrefu bila kuhukumiwa.
UNICEF/Roger LeMoyne
Si haki mtu kukaa gerezani kwa muda mrefu bila kuhukumiwa.

Wajisikiaje kusubiri kunyongwa kwa kosa ambalo hukufanya?

Haki za binadamu

Utekelezaji wa adhabu ya kifo wapungua huku mmoja wa waliosubiria adhabu ya kifo kwa kosa ambalo hakushiriki afunguka

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa imeelezwa kuwa kiwango cha utekelezaji wa adhabu ya kifo kwa mwaka 2018 kilipungua kwa asilimia 31 na kuweka historia katika kiwango cha chini zaidi ya utekelezaji wa adhabu hiyo katika muongo mmoja.

Wafungwa walio kwenye orodha ya kusubiri kunyongwa hadi kufa wanasubiri na katika mahojiano yam waka 2016 na mmoja wa watu waliowahi kukumbwa na kihoro cha kusubiri hatua hiyo, hofu huwa ni ya juu na hali inakuwa mbaya zaidi iwapo unasubiri kunyongwa kwa kosa ambalo hukufanya.

Miongoni mwao ni Edward Mpagi ambaye kwa miaka takribani 20 alikuwa jela akisubiri kunyongwa kwa shutuma za mauaji ambayo hakuyafanya na wala hakuhusika.

Mpagi kutoka Uganda ambaye sasa ana beba bango la kupinga hukumu ya kifo baada ya kupewa msamaha na kutoka jela.

Alizungumza na Flora Nducha katika Makala hii tuliyochapisha tarehe 26 mwezi Septemba 2016 akisimulia ilikuwaje hata roho yake ikawa mkononi..