Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupambana na aina zote za utapiamlo na kukuza ubunifu katika kilimo ndivyo vipaumbele vya juu vya FAO kwa miaka miwili ijayo.

Dkt. Atar Adaha akiwa na mkimbizi kutoka Sudan aliye na mtoto wake mwenye utapiamlo. Ni katika kituo cha kuimarisha lishe cha Hospitali ya Maban kaunti ya Bunj Sudan Kusini.
Credit English (NAMS)
Dkt. Atar Adaha akiwa na mkimbizi kutoka Sudan aliye na mtoto wake mwenye utapiamlo. Ni katika kituo cha kuimarisha lishe cha Hospitali ya Maban kaunti ya Bunj Sudan Kusini.

Kupambana na aina zote za utapiamlo na kukuza ubunifu katika kilimo ndivyo vipaumbele vya juu vya FAO kwa miaka miwili ijayo.

Afya

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO José Graziano da Silva katika hotuba yake ya ufunguzi mkutano wa baraza tendaji la shirika huo ulioanza hii leo mjini Roma Italia, amesisitiza kuwa kwa miaka miwili ijayo FAO itajikita katika kukuza mifumo ya chakula cha lishe na uvumbuzi katika kilimo.

Bwana da Silva amesema, “hatuwezi kuangazia tu katika kupambana na njaa zaidi tena. Lengo namba 2 la maendeleo endelevu linatoa wito wa kutokomeza aina zote za utapiamlo. Na kuna ukuaji katika viwango vya uzito uliopitiliza na utipatwatipwa duniani kote. Wakati njaa imejikitia katika maeneo mahususi, utipwatipwa uko kila mahali. Kwa kweli, tunashuhudia utandawazi wa utipwatipwa.”

Aidha Bwana da Silva ameeleza kuhusu matukio muhimu yajayo ambapo ametaja mkutano wa uhakika wa chakula unaotegemewa kyufanyika baadaye mwezi huu mjini Geneva Uswisi ukiwa umeandalia wan a FAO, shirika la afya duniani WHO na shirika la biashara duniani WTO, uzinduzi wa Muongo wa kilimo cha Kaya utakaofanyika kwenye Makao Makuu ya FAO mwishoni mwa mwezi Mei, semina mbili kuhusu mlo wa afya na uvumbuzi wa kilimo, na pia mkutano wa maktaba wa kimataifa wa kudhibiti uvuvi haramu utakaofanyika mwezi Juni.

Bwana da Silva pia ameeleza kuhusu mafanikio ya FAO kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita katika kupunguza gharama, na kuifanya FAO kuwa na ufanisi zaidi, na inayoleta matokeo bora ikiwa ni pamoja na kuvutia michango zaidi ya hiari.

Vile vile ameonesha ushahidi wa ushirikiano wa FAO na wadau wengine ambapo kutoka wadau 20 na mchango wa dola milioni 28 hadi kufikia zaidi ya wadau 100 wapya kwa sasa wakichangia zaidi ya dola milioni 200. Pia ushiriki wa FAO pamoja na majukwaa ya ushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa vimeongezeka takribani mara mbili tangu mwaka 2012. Hii imeongeza michango kutoka katika mifumo ya Umoja wa Mataifa kwa asilimia 100 kufikia dola milioni 800.