Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulemavu sio kulemaa, ninachohitaji ni kuwezeshwa:Mkulima Gideon Masinde

Udongo wenye rutuba husaidia kilimo bora cha migomba kama vile mkoani Kagera nchini Tanzania
UNDP SGP Panama/Andrea Egan
Udongo wenye rutuba husaidia kilimo bora cha migomba kama vile mkoani Kagera nchini Tanzania

Ulemavu sio kulemaa, ninachohitaji ni kuwezeshwa:Mkulima Gideon Masinde

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ingawa hali ya ulevu hasa wa viungo mara nyingi huleta changamoto kwa muhiska kuanzia  katika maisha ya kawaida na hata katika kujikwamua kiuchumi jambo ambao huwafanya wengi wasio na msaada kuishia kuwa ombaomba, au kukabiliwa na hali ngumu sana. Lakini kama walivyonena wahenga penye njia pana njia , kauli inayothibitishwa na Gideon Malungula Masinde mwenye umri wa miaka 42 ambaye ana ulemavu wa miguu yote na hawezi kusimama wa wala kutembea lakini hakuacha ulemavu wake umlemaze zaidi. 

Masinde baada ya kutokuwa na njia nyingine yoyote ya kujipatia kipato , akachukua hatua ili ajikimu yeye na familia yake na kujikomboa kimaisha kwa kugeukia kilimo tana kile cha asili cha jembe la mkono. Ambacho kutokana na ulemavu wake anakifanya akiwa amekaa na kusota.

Na kwa sababu jembe halimtupi mkulima limesaidia kwa kiasi fulani kwani halali njaa na ameweza kuitunza familia yake japo anakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo vitendea kazi.

Akizungumza na Nicholas Ngaiza kutoka Redio washirika Kasibante FM ya Kagera Tanzania aliyemtembela mkuluma huyo shambani kwake kijiji cha Katembe wilaya ya Muleba mkoani Kagera Tanzania amesema aliamua kukata shauri la kuendesha Maisha yake mwenyewe kwasababu hapendi kuwa ombaomba wakati ana uwezo wa kufanya kilimo hata kama ana upungufu wa viungo kwani ulemavu sio kulemaa.Masinde anaanela ilikuwa hata akakutwa na hali hiyo ya ulemavu

(CLIP YA  NGAIZA & MASINDE)