Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres anafuatilia hali Algeria, apongeza raia kwa utulivu wao

Bendera ya Algeria (Katikati) ikipepea kwenye Umoja wa Mataifa makao Makuu New York
UN Photo/Loey Felipe
Bendera ya Algeria (Katikati) ikipepea kwenye Umoja wa Mataifa makao Makuu New York

Guterres anafuatilia hali Algeria, apongeza raia kwa utulivu wao

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ametambua na kuzingatia  hatua ya kujiuzulu kwa rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu kwa vyombo vya habari, bwana Guterres amewapongeza watu wa Algeria kwa kuonyesha ukomavu na utulivu wakati wa maandamano ya kutaka  mabadiliko. Aidha taarifa hiyo imeelezea matarajio ya Guterres kuona mabadiliko ya uongozi yenye amani na ya kidemokrasia yanayoonyesha matakwa ya watu wa Algeria.

Halikadhalika Katibu Mkuu amerejelea kuweka wazi kuhusu utayari wa Umoja wa Mataifa kuendelea kuunga mkono Algeria katika mchakato wa mabdiliko ya mamlaka ya kidemokrasia.

Rais Bouteflika alichaguliwa mwaka 1999 kwa mara ya kwanza wakati huo akiungwa mkono na vyombo vya usalama hivyo amekaa madarakani kwa takribani miaka 20. Rais huyo mwenye umri wa miaka 82 atang'atuka rasmi madarakani April 28 mwaka huu.