Kampeni ya kuwalinda wasichana na wavulana katika vita yalizinduliwa:Gamba

2 Aprili 2019

Kampeni mpya ya kuchagiza uelewa na kuboresha hatua za kuwalinda watoto walioathirika na migogoro ya silaha imezinduliwa leo kwenye mkutano maalum katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.

Akizindua kampeni hiyo kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kwa ajili ya watoto na migogoro ya silaha Virginia Gamba, amesema “kukiwa na watoto wengi zaidi wanaoathirika na ukatili katika maeneo ya vita kote duniani tunahitaji kuongeza haraka juhudi zetu ili kuelimisha kuhusu wajibu mkubwa ninaouwakilisha , wa aina sita za ukiukwaji mkubwa na kuongeza mara mbili kazi za kuelimisha ili kuhakikisha hatua zinachukuliwa na pande zote katika mzozo na kuwapa Watoto ulinzi wanaostahili.”

Ameongeza kuwa katika miaka mitatu ijayo kampeni hiyo iliyopewa jina “Chukua hatua kulinda watoto walioathirika na mgogoro” itakuwa ikitafuta kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia na jumuiya ya kimataifa ili kusaidia hatua zilizotengwa kwa ajili ya kukomesha na kuzuia ukiukwaji mkubwa wa haki za Watoto wakati wa vita.

Bi Gamba amesema msaada huu utajumuisha elimu ili kufikia kuridhia mkataba wa kimataifa au kuidhinisha makubaliano ya kimataifa kama kipengele cha chaguo kwenye mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto kwa watoto walio katika migogoro ya silaha, kanuni za Paris, azimio la shule salama na kanuni za Vancouver.

Kampeni hiyo pia itatia msukumo katika utekelezaji wa hatua za mipango iliyotiwa saini baina ya Umoja wa Mataifa na pande zinazohusika katika migogoro , lakini pia ushiriki mkubwa na pande zote zilizoorodheshwa katika migogoro ili kuongeza mipango mingine ya hatua na ahadi ya kukomesha ukiukwaji wa haki za Watoto. Bi. Gamba amesisitiza kuwa “Wakati tukifufua ushiriki wet una hatua za kukomesha ukiukwaji wa haki ni muhimu kampeni ikajikita pia katika miradi iliyoanzishwa ili kuzuia ukiukwaji huo.” Eneo linguine la kupewa kipaumbele amesema ni “kuelimisha kuhusu umuhimu wa kutoa huduma zinazostahili kwa Watoto walioathirika na vita.”

Bi Gamba ambaye ameshukuru kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa kwa kampeni hiyo kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa kama la kuhudumia Watoto UNICEF nan chi wanachama amesema “sio tu kwamba itatoa hakikisho la sauti za wavilana na wasichana Zaidi kusikika bali pia kwa pamoja tunaweza kuchukua hatua kuwalinda watoto zaidi.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter