Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sikujua lolote kuhusu wakimbizi hadi nilipokutana na Jean:Msamaria Annita 

Mapigano ya kikabila huko DRC yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makwao, mathalani katika jimbo la Kalemie ambapo wakazi wake pichani wakionekana kwenye sintofahamu.
UNHCR/Colin Delfosse
Mapigano ya kikabila huko DRC yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makwao, mathalani katika jimbo la Kalemie ambapo wakazi wake pichani wakionekana kwenye sintofahamu.

Sikujua lolote kuhusu wakimbizi hadi nilipokutana na Jean:Msamaria Annita 

Wahamiaji na Wakimbizi

Miaka minne iliyopita msamaria mwema Annita Sangili raia wa Kenya mwenye umri wa miaka 43 alikutana na mkimbizi kwenye basi maarufu kama matatu jijini Nairobi , mkimbizi aliyelazimika kulala kwenye basi kwa kukosa kwa kwenda akisaka msaada wa kumfikisha kanisani ilia pate hifadhi.

Jean Petil aliyekimbia vita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 16 tu, alikutana na nyota ya jaha baada ya usiku kucha kulala ndani ya matatu akitarajia kufika kanisani alikoelzwa angepewa hifadhi. Nyota hiyo si nyingine bali ni Annita Sangili amabye anasema alipozungumza na Jean aliwiwa kumsaidia, “Jean alionekana kuchanganyikiwa nilipomuona kwenye basi, na moyo wangu ukahisi huruma ya kumsaidia kufika kanisani alikolala kwa usiku mmoja.”

Hata hivyo Annita aliguswa zaidi na hali ya Jean ndipo akaamua kujitolea kumsaidia kwa kumpa hifadhi nyumbani kwake  akikumbuka wosia wa baba yake”Baba yangu alinifunza daima kushirikiana na kusaidia wenye uhitaji, na bila shaka Jean alihitaji mahali pa kukaa.” 

Na kwa miaka mine sasa Annita anaishi na Jean nyumbani kwake kwenye makazi ya Umoja jijini Nairobi katika nyumba ya vyumba viwili akimsaidia kwa kila kitu ikiwemo nauali za kumpeleka kila mara kwenye ofisi za shirika la Umojawa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kufanyiwa usahili wa kupewa hadhi ya ukimbizi.

Baada ya miaka mitatu ya usahili sasa Jean amepewa hadhi ya ukimbizi na amasema yote haya yamewezekana kwa ajili ya wema na ukarimu wa Annita

“Annita ni kama mama na dada kwangu, amenisadia sana na anaendelea kunisaidia kutafuta kazi za mikono ili niweze kuishi.”

Baada ya kukimbia DRC, Jean alikwenda Burundi lakini akalazimika kukimbia tena yalipozuka  machafuko Burundi na akajikuta Afrika Kusini  na hatimaye Kenya. 

Jean walizaliwa wawili na dada yake ambaye hivi sasa ni mkimbizi nchini Tunisia na wazazi wao wote wawili waliuawa.

UNHCR inasema inashirikiana kwa karibu na serikli ya Kenya ili kuwapa vibali vya kuweza kufanya kazi wakimbizi walioko mijini akiwemo Jean.