Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vya IDAI vinaongezeka , huku mlipuko kipindupindu waongeza hofu Msumbiji:OCHA

Umoja wa Mataifa Msumbiji tayari unawasaidia walioathirika na mafuriko yaliyotokana na kimbunga IDAI
UN Mozambique
Umoja wa Mataifa Msumbiji tayari unawasaidia walioathirika na mafuriko yaliyotokana na kimbunga IDAI

Vifo vya IDAI vinaongezeka , huku mlipuko kipindupindu waongeza hofu Msumbiji:OCHA

Msaada wa Kibinadamu

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA , idadi ya vifo vilivivyosababishwa na athari za kimbunga Idai nchini Msumbiji imeongezeka na kufikia 493.

Shirika hilo linasema na mlipuko wa kipindupindu ulioripotiwa katika eneo la Nhamatande umeongeza tisho ingawa tayari vituo 9 vya matibabu vimeanzishwa kwenye jimbo la Beira na maeneo mengine.

Hadi sasa watu 140,000 wametawanywa katika maeneo 161 kwenye majimbo ya Sofala, Manica, Zambezia, na tete na 7400 kati yao wameelezewa kuwa wako hatarini na wasiojiweza kwa mujibu wa serikali.

Mashirika ya Umoja wa mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF, la afya WHO, la mpango wa chakula WFP na mashirika mengine ya kimataifa kama COSACA na World Vision yametoa taarifa ya pamoja kuhusu lishe kwa watoto wachana katika juhudi za kukabiliana na hali nchini Msumbiji.

Mtazamo wa hali halisi

Mpaka sasa mashirika hayo ynasema visa 271 wa kipindupindu vimeripotiwa Beira na mlipuko mpya umeripotiwa Nhamatande.

Wadau wa afya wanajikita katika kuimarisha ufuatiliani wa magonjwa na kudhibiti mlipuko wa kipindupindu. Maaandalizi ya chanjo ya kipindupindu iliyopangwa kuanza wiki ijayo yanaendelea huku vituo tisa vya matibabu vimeanzisha na saba kati ya vituo hivyo tayari bvimeanza kufanya kazi vikiwa na takribani vitanda 400.

Wakatihuohuo kwenye jimbo la Manica ongezeko la visa vya malaria limeripotiwa katika wilaya mbalimbali na hatari ya mlipuko wa kipindupindu ni kubwa katika wilaya nyingi zilizoathirika na Idai.

Hatua zilizochukuliwa hadi sasa

OCHA inasema hadi sasa Zaidi ya watu 241,000 wamefikiwa na msaada wa chakula wakiwemo 10,000 ambao wanapata chakula maalum kilichoanza kusambazwa mjini Beira. Na mkakati wa kufuatilia usambazaji wa msaada wa chakula kwa njia ya anga unaendelea.

Kufuatia tathimini ya mahitaji ya chakula katika majimbo ya Nhamatanda na Chimoio tarehe 28 Machi WFP imeandaa chakula tayari kwa kugawa kwa watu 8,000 katika miji ya Mutichira na kwa jamii zingine katikati ya ukingo wa kaskazini wa Mutichira na Kusini wa mto Pungwe.