Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nina matumaini ya mustakabali wa Libya:Guterres

Mkutano na waandishi wa habari wa Quartet kuhusu Libya tarehe 31 Machi 2019 mjini Tunis Tunisia. Kutoka kulia Federica Mogherini, mwakilishiwa EU kuhusu mambo ya nje na sera za usalama, Ksatibu Mkuu wa UN Antonio Guterres, Ahmad Abulgheit Katibu mkuu wa m
UN Photo/Ahmed Gaaloul
Mkutano na waandishi wa habari wa Quartet kuhusu Libya tarehe 31 Machi 2019 mjini Tunis Tunisia. Kutoka kulia Federica Mogherini, mwakilishiwa EU kuhusu mambo ya nje na sera za usalama, Ksatibu Mkuu wa UN Antonio Guterres, Ahmad Abulgheit Katibu mkuu wa m

Nina matumaini ya mustakabali wa Libya:Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ana matumaini kwa ajili ya suluhu ya mgogoro wa miaka minane wa Libya baada ya kushiriki mkutano wa ngazi ya juu leo Jumamosi mjini Tunis Tunisia.

Mkutano huo wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu au Arab League umejumuisha maafisa kutoa nchi za Kiarabu, Muungano wa Ulaya na Muungano wa Afrika.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Katibu Mkuu amesema “ Baada ya kuwa na mkutano wenye ufanisi na washirika wetu kuhusu Libya Quartet, neno ambalo linaelezea ninachohisi kuhusu Libya hivi leo ni tumaini. Hali ni ngumu lakini ni muhimu kutumia fursa hii kusaidia zaidi suluhu inayoongozwa na Walibya.”

Mkutano huo mjini Tunisia umemjumuisha Federica Mogherini mwakilishi wa Muungano wa Ulaya kwa mambo ya nje na sera za usalama, Ahmad Abulgheit Kastibu mkuu wa Aran League, Moussa Faki , mwenyekiti wa tume ya Muungano wa Afrika na Ghassan salame mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya.

Baada ya mkutano huo kumefanyika mkutano na waandishi wa habari na katika ukurasa wake wa Twitter Bwana. Salame ametoa wito kwa watu wa Libya “Msipoteze fursa hii ya mapendekezo yaliyopitishwa wakati wa mkutano huu wa ngazi ya juu na msifunge dirisha hili la kujenga taifa lenye Umoja, la kiraia, lililo huru, lenye uwezo na usawa."
Kwa muda mrefu tangu kuangushwa kwa utawala wa dikteta Muammar Gaddafi mwaka 2011 taifa hilo la Afrika  lililo katika bahari ya  Mediterranea limekuwa likigombewa na makundi yenye silaha ambayo yamesababisha kuporomoka kwa uchumi, miundombinu na usalama nchi nzima. Leo Libya imeanza uchaguzi wa majimbo katika manispaa tisa nchini humo.