Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuwezesheni kuwafikia wahitaji Hajjah yemen:WFP

Nafaka zilizohifadhiwa huko Dhubab, jimbo la Taiz nchini Yemen. WFP kwa muda mrefu ilikuwa imeshindwa kufikia nafaka iliyokuwa imehifadhiwa kwenye kinu cha kusagisha unga cha Red Sea na hivyo kutia shaka pengine itakuwa imeoza
Giles Clarke/OCHA
Nafaka zilizohifadhiwa huko Dhubab, jimbo la Taiz nchini Yemen. WFP kwa muda mrefu ilikuwa imeshindwa kufikia nafaka iliyokuwa imehifadhiwa kwenye kinu cha kusagisha unga cha Red Sea na hivyo kutia shaka pengine itakuwa imeoza

Tuwezesheni kuwafikia wahitaji Hajjah yemen:WFP

Amani na Usalama

Wakati mzozo wa Yemen ukiingia mwaka wa tano, maeneo ambako kuna mahitaji zaidi hayafikiki kwa ajili ya kuwasilisha msaada limesema Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi msemaji wa WFP Herve Verhoosel amesema WFP inahitaji kufikia watu walioko hatarini kwa uhuru bila vizuizi vyovyote ili kuhakikisha hali ya njaa haiwi mbaya zaidi.

Jana tarehe 25 Machi WFP imeelezea wasiwasi wake kufuatia ripoti za kuongezeka kwa uhasama katika maeneo kadhaa ya mji wa Hodeidah ikiwemo katika mtaa wa Sana’a uwanja wa ndege wa Hodeidah, chuo na Kilo na maeneo mengine. WFP imeongeza kuwa usalama ni lazima ili kuhakikisha uwasilishaji wa misaada inayotolewa na WFP na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa.

Bwana Verhoosel ametolea mfano jimbo la Hajjah moja ya maeneo kunakoshuhudiwa uhaba wa chakula, ongezeko la ukatili unahatarisha maelfu ya watu kukabiliwa na njaa kubwa ambapo katika kipindi cha miezi sita, idadi ya watu waliofurushwa kutokana na ongezeko la ukatili imeongezeka sana kutoka 203,000 hadi watu takriban 420,000.

Kwa mujibu wa shirika hilo kaya 11,000 zimefurushwa katika jimbo la Hajjah tangu kuzuka kwa mapigano mapema mwaezi huu wa Machi na shirika hilo limetoa mgao wa chakula kwa familia 5,000 na bado mgao wa chakula unaendelea.

WFP na wadau wake hawajaeweza kufikia wilaya nne karibu na mpaka wa Saudia kwa sababu ya ongezeko la machafuko hususan wilaya ya Harad, Mustaba, Midi na Hayran ambako kuna takriban watu 50,000 walio katika hatari ya kufariki kutokana na njaa.