Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japo majanga mengine hayaepukiki, tahadhari ni muhimu:UNEP

Kufuatia ,mabadiliko ya tabianchi ukame wa mara kwa mara unatishia usalama wa chakula.
©FAO/Giulio Napolitano
Kufuatia ,mabadiliko ya tabianchi ukame wa mara kwa mara unatishia usalama wa chakula.

Japo majanga mengine hayaepukiki, tahadhari ni muhimu:UNEP

Tabianchi na mazingira

Hivi karibuni katika maeneo mengi ya Afrika Mashariki hali ya joto la kupindukia, mafuriko na kuchelewa au kukosekana kwa mvua imekuwa ni gumzo kubwa huku wakulima wakihaha kuokoa mazao yao.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira vyote hivi ni dalili dhahiri ya mabadiliko ya tabianchi na hivyo kuzitaka nchi kuchukua hatua stahili ili kuhimili na pia kuwanusuru wananchi wake pindi majanga ya asili yanapozuka. Ili kufahamu zaidi kuhusu mabadiliko haya ya tabia nchi yanayoeleta zahma kubwa ikiwemo ukame , mafuriko na hata vimbunga kama IDAI mwandishi wetu Stella Vuzo wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam Tanzania amezungumza na Bi Clara Makenya mratibu na afisa wa UNEP nchini humo

(MAHOJIANO YA STELLA VUZO NA CLARA MAKENYA)