WHO yatoa msaada ya dawa na vifaa vya dharura Gaza
Shirika la Afya Duniani (WHO) hii leo limetoa msaada wa dawa na vifaa muhimu kwa badhi ya vituo vya huduma ya dharurua Gaza ili kukabiliana mahitaji ya kiafya katika ukanda wa Gaza .
Msaada huo ambao ni ukarimu wa nchi za muungano wa Ulaya utawezesha vituo 10 vya dharura vinavyoendeshwa na wizara ya afya ya Palestina kwa ushirikisano na shirika la hilali nyekundu, Kuweza kutoa huduma za afya hususan kwa majeruhi wa viungo katika maandamano.
Dr Gerald Rockenschaub, ambaye ni mkuu wa ofisi ya WHO Palestina ameshukuru Muungano wa nchi za Ulaya kwa msaada katika Ukanda wa Gaza, akiongeza kuwa
"Upungufu wa rasilimali na huduma muhimu za afya kwa majeruhi wa viungo wa muda mrefu unaweza kusababisha ulemavu au hata matokeo mabaya ya kiafya”.
Aidha WHO na mashirika ya afya wanafanya kazi pamoja ili kuhakikisha kuwa huduma za dharura TSPs zina uwezo wa kuboresha afya ya wagonjwa, kupunguza hatari ya matatizo ya kuzuia maumivu au kupoteza viungo, na kuhakikisha matokeo bora ya afya.
WHO imesema msaada huo ni muhimu sana kutokana na idadi kubwa ya majeruhi yatokanayo na majeraha ya risasi za moto, hiyvo inafanya jitihada kuimarisha ngazi zote za usimamizi wa majeraha na kuhakikisha kuwa kabla ya kufikishwa hospitali, timu za huduma za dharura TSP zina dawa muhimu na vifaa vya matibabu ya awali kwa waliojeruhiwa.
Msaada huo utaweza kusaidia mahitaji ya watu 120,000 wasio na majeraha ya kutisha sana au wagonjwa 20,000 waliojeruhiwa vibaya. Mbali na dawa na vifaa vya matibabu, WHO imetoa mahema 4 kwa kila TSP ili kuhakikisha timu zina nafasi ya kutosha kutibu wagonjwa wenye shida tofauti. Vituo vitano vimepewa jenereta zinazoendesha huduma za msingi, kama vile utoaji wa hewa ya oksijeni kwa wagonjwa.
WHO pia imetoa mahema yanayoweza kutengenezwa ambayo yanaweza kusimamishwa ndani ya dakika chake wakati wa dharura na pia yanayoweza kuhamishwa haraka kwa maeneo mbadala ili kutibu watu wanaohitaji hudma za dharura.
Mbali na mahitaji makubwa yaliyotekelezwa, WHO imetoa wito wa dola milioni 5.3 wakati huu ambapo wanajiandaa na maadhimisho ya mwaka mmoja ya maandamo yajayo ambayo yanaweza kusababisha majeruhi zaidi.
WHO na washirika wa kikundi cha afya walitengeneza mpango wa dharura kushughulikia mahitaji ya afya ndani ya masaa 96 ili kuzuia kifo na ulemavu. Ili kuongeza zaidi ngazi zote za utunzaji wa majeraha.