Sudan Kusini yazindua kampeni ya chanjo ya homa ya manjano jimboni Gbudue:WHO

25 Machi 2019

Wizara ya afya ya Sudan Kusini kwa ufadhili wa shirika la afya duniani, WHO na wadau wengine, wamezindua kampeni ya chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya manjano katika eneo la Sakure, kaunti ya Nzara jimboni la Gbudue ili kuwachanja watu 19,578 wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka 65.

Taarifa iliyotolewa mjini Yambio Sudan Kusini hii leo imesema, kampeni ya chanjo inafuatia kutokana na mlipuko wa ugonwa huo tarehe 29 mwezi novemba mwaka 2018 ambapo jumala ya maabara tatu zilithibitishauwepo wa ugonjwa huo japo hakuna vifo ambavyo vimeripotiwa baada ya uchunguzi kufanyika katika eneo la Sakure payam.

Mwezi Disemba 2018, timu yenye watalaamu wa aina mbalimbali wakiwemo watafiti wa magonjwa, maafisa afya ya jamii, wataalamu wa wadudu waambukizao magonjwa pamoja na wataalamu wa maabara na wale wa mawasiliano, walifanya uchunguzi wa kina kuangalia ukubwa wa mlipuko, kutambua wadudu wasambazaji wa ugonjwa, kutathimini hatari iliyopo na kuangalia namna ya kuudhibiti ugonjwa huo ili usienee zaidi.

Chanjo ya homa ya manjano ni moja ya mkakati wa kidunia wa kutokomeza mlipuko wa homa ya manjano ifikapo mwaka 2026, anasema Dkt Olushayo Olu, mwakilishi wa WHO Sudan Kusini.Chanjo hiyo inasaidia kuwaokoa watu wengi na hatari ya kukumbwa na virusi vya homa ya manjano katika hatua za muda mfupi na baadaye muda mrefu.

Ugonjwa wa homa ya manjano unatokana na aina ya virusi vinavyosambazwa na mbu wanaoukuwa wameambukizwa ugonjwa huo. Dalili zake ni pamoja na homa, kuumwa kichwa, macho kubadilika rangi na kuwa ya njano, maumivu ya misuli, kizunguzungu, kutapika na kuchoka mwili. Idadi ndogo ya wagonjwa wanaoambukizwa na ugonjwa huo wanaweza kuonesha dalili kali na kwa wastani nusu yao hupoteza maisha ndani ya siku 7 hadi 10.

Homa ya manjano huweza kuanza kujitokeza ndani ya siku tatu hadi sita mara baada ya maambuki. Watu wengi hawapati dalili za ugonjwa huu lakini pale zinapojitokeza, mara nyingi ni homa, misuli kuuma na maumivu ya mgogo, kichwa, kukosa hamu ya kula, kizunguzungu na kutapika. Katika baadhi ya wagonjwa dalili hutoweka baada ya siku tatu hadi nne.

Mara ya mwisho kwa Sudan Kusini kushambuliwa na mlipuko mkubwa wa homa ya manjano ilikuwa mwezi Mei mwaka 2003 katika mkoa wa Imatong, kaunti ya Torit ambapo watu 178 waligundulika kuwa na ugonjwa huo na watu 27 wakapoteza maisha.

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud

Fuatilia Habari: Habari zilizopita za Mada Hii

Mlipuko wa homa ya manjano wauwa watu zaidi ya 40 Nchini Uganda

Shirika la afya duniani WHO linaisaidia wizara ya afya ya Uganda kukabiliana na mlipuko wa homa ya manjano ambao umeshakatili maisha ya watu zaidi ya 40.

WHO linatarajiwa kuanzisha uchanjaji wa homa ya manjano katika Guinea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kwamba, litajihusisha na uchanjaji wa watu 60,500 dhidi ya homa ya manjano katika Guinea, kuanzia tarehe 26 Januari (2009) baada ya watu wawili kugundulikana waliambukizwa na maradhi haya maututi katika wilaya ya Faranah, iliopo katika Guinea ya kati, karibu na Mto Niger. Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na maabara ya kikanda ya Taasisi ya Pasteur, Dakar, Senegal hatua hii inachukuliwa mapema ili kudhibiti haraka ugonjwa usije ukaripuka na kuenea kwenye taifa hilo husika. ~