Athari za IDAI Msumbiji ni kama bomu linalosubiri kulipuka:IFRC

25 Machi 2019

Atahari za kimbiunga IDAI Kusini mwa Afrika ikiwemo Zimbabwe na Malawi ni kubwa lakini nchini Musumbiji ni sawa na bomu linalosubiri kulipuka hususani katika masuala ya afya na usafi. 

Hayo yameelezwa na Rais wa chama cha msalanba mwekundu Elhadj As-Sy akizungumza hii leo na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis baada ya kuzuru Msumbiji na kujionea hali halisi. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takriban watu 1000 wamepoteza maisha na idadi huenda ikaongezeka huku wengine zaidi ya milioni 1.8 wameathirika wakikosa huduma za msingi kama vile malazi, maji safi na huduma za afya ambazo wanazihitaji haraka

(SAUTI YA ELHADJ AS SY)

“Wakati kukiwa na watu wengi walioathirika na mafuriko katika kiwangi tunchokishuhudia hivi sasa Msumbiji na hali halisi ambayo ni mbaya katika vituo vya muda na malazi ya dharura kwa halika tumeketi katika bomu la maji, na usafi linalotarajiwa wakati wowote kulipuka”

WFP/Andrew Chimedza
Kimbunga Idai kimesababisha uharibifu kwa asimia 90 katika jiji la Beira.

Akifafanua zaidi amesema

(SAUTI YA ELHADJ AS SY )

“Watu elfu 3000 katika shule yenye madarasa 15 na vyoo sita tu mjini Beira ni chachu ya zahma na magonjwa yatokanayo na maji yanaweza kulipuka kama kipindupindu, homa ya matumbo na tunaweza kuwa na visa zaidi vya malari. Hivyo kuchukua hatua haraka kwa ajili ya maji, usafi na maji safi ni muhimu sana.”

Mashirika mbalimbali ya kitaifa, kimataifa na ya Umoja wa Mataifa likiwemo la afya WHO, la wakimbizi UNHCR , uhamiaji IOM, la mpango wa chakula WFP,  la kuhudumia watoto UNICE na la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA wanafanya kila liwezekanalo kukidhi mahitaji ya dharura ya waathirika ikiwemo ya chakula, maji, madawa, na malazi.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud