Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN apokea kuundwa kwa serikali ya pamoja CAR.

Wananchi wakiwa na bendera ya Jamhuri ya Afrika ya Kati nchini mwao.
MINUSCA
Wananchi wakiwa na bendera ya Jamhuri ya Afrika ya Kati nchini mwao.

Katibu Mkuu wa UN apokea kuundwa kwa serikali ya pamoja CAR.

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, amekaribisha uundwaji wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR kwa mujibu wa mkataba wa amani na upatanisho uliotiwa saini mjini Bangui tarehe 6 mwezi Februari mwaka huu. 

Katibu Mkuu Guterres anaupongeza mchango wa uongozi wa muungano wa Afrika hususani katika kukalimilisha mazungumzo kuhusu CAR yaliyofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia kuanzia tarehe 18 hadi 20 mwezi huu wa Machi kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa.

Bwana Guterres anawasihi wote waliotia saini katika makubaliano ya kisiasa kwa ajili ya amani na upatanisho kuzingatia kanuni zilizikubaliwa hususani kukataa vurugu na kuheshimu haki za binadamu na utu. Pia amewasihi wote walioingia makubaliano ya amani kuharakisha utekelezaji wake.

Vile vile Katibu Mkuu amekumbushia ahadi ya Umoja wa Mataifa kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya kati na akatoa wito kwa wadau wote kuendelea kuwasaidia watu na serikali ya CAR katika juhudi zao za kupata amani ya kudumu nchini mwao.