Bado usawa ni nadharia duniani:UNDP Ripoti

22 Machi 2019

Bado kuna kiwango kikubwa cha kutokuwepo na usawa duniani huku maisha na mustakabali wa watoto wanaozaliwa katika familia za nchi masikini na wale wanaozaliwa katika nchi Tajiri ukiwa na tofauti kubwa, kwa mujibu wa ripota ya maendeleo ya binadamu duniani iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP.

Ripoti hiyo iliyojikita katika “pengo la usawa” inasema katika jamii zote mifumo ya muda mrefu ya kutokuwepo kwa usawa inaendelea na pengo linazidi kupanuka katika aina mpya za maisha. Kwa mujibu wa UNDP ripota hiyo ya maendeleo ya binadamu kwa mwaka 2919 inaangalia kwa kina uelewa wa mifumo ya kutokuwepo kwa usawa na la msingi zaidi katika maisha ya wat una nini kinachochangia.

Ripoti hiyo itakayotolewa katika robo ya mwisho ya mwaka huu itatoa taswira halisi ya mifumo mingi ya kutokuwepo usawa ambayo imetawala katika karne hii ya 21. Akifafanua Zaidi mkurugenzi wa ofisi ya ripota ya Maendeleo ya binadamu kwenye shirika la UNDP Pedro Conceição, amesema “Wakati watu wengi wanaamini kwamba kutokuwepo usawa ni muhimu , kuna makubaliano madogo sana ya kwa nini ni muhimu na nini kifanyike kuhusu hilo.

Tunahitaji kunoa vipimo ili kuweka bayana zaidi kutokuwepo na usawa kukoje, na kuwa na uelelewa mkubwa wa jinsi gani pengo la usawa litabadilika kutokana na mabadiliko ya kimazingira ,ya kijamii na kiuchumi ambayo yanashuhudiwa kote duniani hadi wakati huo ndio tutaweza kuwa na chaguo la kuundasera ambazo zitakabiliana na hali hiyo.”

Ripoti itaenda mbali z aidi yay a kuangalia tofauti za usawa katika pengo lakipato, pia itaangalia pengo la usawa katika masuala mengine kama afya, elimu, fursa za teknolojia na uelewa wa misikukosuko kama ya kiuchumi na mabadiliko ya hali ya hewa. Ripoti hiyo itatumia njia na takwimu mpya ambazo zitaelezea kwa njia ambayo si rahisi kwa mbinun zingine jinsi pengo la usawa linavyoathiri maisha ya wat una pia itatathimini kwa kina ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 203, mafanikio ya ajenda hiyo na zaidi.

Bwana Conceição amesema “sasa hivi duniani tunashuhudia mabadiliko makubwa katika maendeleo ya binadamu kwa mfano katika nchi nyingi mapengo yameanza kiuzibwa tunapozungumzia fursa za elimu ya msingi lakini tofauti baina ya Watoto wanaotoka familia masikini na familia tajiri pengo linaongezeka katika maisha ya awali na ubora wa elimu. Mapengo haya ya usawa yatakuwa na athari kubwa maishani hususanukizingatia mabadiliko ya haraka ya teknolojia ambayo yanauwezekano mkubwa  wa kuathirti masoko ya ajira.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud