Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirika wa Kusini-Kusini ni muhimu kwa vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:Guterres

Katibu Mkuu  Anotnio Guterres akihutubia kwenye mkutano wa kusini kusini  mjini  Buenos Aires, Argentina.
UNIC Buenos Aires/Mariano Solier
Katibu Mkuu Anotnio Guterres akihutubia kwenye mkutano wa kusini kusini mjini Buenos Aires, Argentina.

Ushirika wa Kusini-Kusini ni muhimu kwa vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:Guterres

Masuala ya UM

Ushirika wa Kusini-Kusini ni muhimu sana katika vita vya kimataifa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo Jumatano kwenye ufunguzi wa mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu ushirika wa Kusini-Kusini unaoendelea mjini Buenos Aires nchini aregentina.

Antonio Guterres amewakumbusha washiriki ambao ni viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na viongozi wa asasi za kiraia kwamba mkutano wa BAPA+40 kama unavyofahamika kwa kifupi utaimarisha mazingira ya ajenda iliyowekwa kwa mara ya kwanza miaka 40 iliyopita ambayo ilipitisha mjini Buenos Aires mkakati wa hatua wa kuchagiza na kutekeleza ushirikiano wa kiufundi miongoni mwa mataifa yanayoendelea (BAPA).

Guterres amesema wiki hii ni fursa ya kurejea ahadi za kuchukua hatua, maendeleo na kuimarisha mundo wa ushirikiano wa Kusini-Kusini  miongoni mwa mataifa ya upande wa Kusini pamoja na kuimarisha mifumo na nyenzo , kuopanua wigo wa uwazi na kuimarisha uwajibikaji. Ameongeza kuwa “ BAPA imebadili mwelekeo wa ushirikiano wa kimataifa. Umeainisha thamani ya ushirika tofauti kwa kuzingatia ubadilishanaji wa taaluma na teknolojia miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na changamoto sawa za maendeleo.”. Pia amesema ushirikiano huo utawezesha nchi zinazoendelea kujifunza kutoka miongoni mwao na kupiga hatua haraka, kuziba pengo na kujenga jamii zenye mnepo na jumuishi.

Katibu Mkuu Antonio Guterres akiwa na rais wa Argentina Bw. Mauricio Macri, kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kusini kusini mjini Buenos Aires, Argentina.
UNIC Buenos Aires/Mariano Solier
Katibu Mkuu Antonio Guterres akiwa na rais wa Argentina Bw. Mauricio Macri, kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kusini kusini mjini Buenos Aires, Argentina.

 

Masuala matano, suluhu nyingi

 Katibu Mkuu amefafanua changamoto kubwa ambazo viongozi wa dunia waliokusanyika wanaweza kusaidia kuyashughulikia ambayo ni muhimu katika kufikia ajenda ya mwaka 2030 ya malengo ya ameendeleo endelevu na mkataba wa Paris wa 2015 unaozitaka nchi kuhakikisha ongezeko la joto duniani linasalia chini ya nyuzi joto mbili .

Mosi Katibu Mkuu amesema kuna ongezeko la pengo la kutokuwepo usawa miongoni na ndani ya nchi wanachama , hali ya kutoaminiana inaongezeka duniani kote na pia pengo la kutokuwa na haki linaongezeka.

Pili Guterres amesema mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi yanazidi kuchukua sura mpya kwani “2018 ilikuwa ndio mwaka wenye joto Kali la kupindukia katika historia na majanga ya asili yanaathiri karibu kila kanda” amewaamboia nchi wanachama kwamba ni lazima kusongesha juhudi za kitaifa za kuchangia katika vita hivi ifikapo mwaka 2020, kwa kuzingatia kupunguza gesi ya viwandani kwa asilimia 45 katika muongo ujao.

Amehimiza kwamba “Ushirika wa Kusini-Kusini utakuwa muhimu sana katika kuhakikisha msaada na kubadilishana uzoefu mzuri , kuimarisha mnepo kwa nchi zinazoendelea na katika jamii zinazokabiliwa na athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi.”

 

Katibu Mkuu Guterres kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kusini kusini Buenos Aires
UN News Photo
Katibu Mkuu Guterres kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kusini kusini Buenos Aires

 

Guterres ameongeza kuwa ushirika wa Kusini-Kusini unaeweza kusaidia katika mabadiliko ya uchumi kutegemeana na mafuta mbadala, mikakati ambayo inachagiza maendeleo endelevu na ulinzi wa mazingira.

Tatu katika orodha ya mambo hayo matano ni haja ya kuboresha miundombinu hususan mijini hasa kwa kuzingatia kwamba mahitaji ya nishati katika ukanda mzima wa Kusini yanaongezeka “ takribani aslimia 60 ya eneo linalotarajiwa kuwa miji ifikapo mwaka 2030 bado halijajengwa Na tusipolizingatia hili tutajikuta tumejigfunga katika mustakbali wenye kiwango kikubwa cha hewa chafuzi ya itakayokuwa na athari kubwa sana duniani.”

Nne Katibu Mkuu amesema” ingawa kumekuwa na hatua zilizopigwa katika kufikia usawa wa kijinsia kwa miaka kadhaa sasa lakini pengo la usawa linaongezeka.”Na hili linatuathiri sote kwani katika mahali ambapo wanawake wanauwakilishi mzuri katika siasa tunaona mabadiliko katika hifadhi ya jamii na ongezeko katika matumizi ya maendeleo.”Amesema kwamba “pale ambapo mwanamke ana fursa ya kupata ardhi na mikopo mavuno yanaongezeka na pale ambapo wasichana wanapata elimu wanachangia zaidi katika jamii na kuvunja mzunguko wa umasikini.”

Tano na mwisho Guterres amesema taasisi za kimataifa zinahitaji kuongeza juhudi kuzisaidia nchi zinazowakilishwa Buenos Aires “Ushirika wa Kusini-Kusini umebadilkika kwa kiasi kikubwa  katika muongo uliopita lakini taasisi za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa haziendi sambamba na mabadiliko hayo. Hata hivyo amezishukuru nchi waanchama kwa kutambua jukumu la Umoja wa Mataifa kwa azimio la mkutano huo ambalo litapitishwa siku ya Ijumaa.

Katibu Mkuu ameonya kwamba ushirika wa Kusini-kusini hauwezi kuwa mbadala kwa msaada rasmi wa maendeleo au kuchukua nafasi ya wajibu w anchi zilizoendelea na kwamba ni lazima vijana, asasi za kiraia , sekta binafsi, wanzuoni na wengine kushirikishwa katika kujenga ushirika bunifu.

Amesisitiza kwamba ushirika huo ni fursa kwa nchi zote za Kusini kufaidika ikiwemo nchi zenye maendeleo dunia.