Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa chakula waleta manufaa kwa Watoto wa shule Guatemala

Mlo wa shuleni ukiandaliwa na akina mama wanoajitolea ambao wamesomea masuala ya lishe, kwa maana ya mandalizi kwa kuzingatia vigezo vya usafi na stadi zingine.
©Pep Bonet/NOOR for FAO
Mlo wa shuleni ukiandaliwa na akina mama wanoajitolea ambao wamesomea masuala ya lishe, kwa maana ya mandalizi kwa kuzingatia vigezo vya usafi na stadi zingine.

Mradi wa chakula waleta manufaa kwa Watoto wa shule Guatemala

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mradi wa kulisha watoto shuleni nchini Guatemala umefikia shule zaidi ya 400 na unalenga kuogeza idadi ya shule zinazonufaika hadi 35,000 katika siku za usoni lengo likiwa kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria shule limesema shirika la chakula na kilimo FAO.

Kwa mujibu wa FAO mradi huo  ambao ni wa kuendesha kilimo mashuleni na mazao yanayopatikana kuwa ndio mlo unatoa fursa kwa watoto ambao hawajiwezi kuhudhuria shule na kupata mlo shuleni jambo ambalo limekuwa changamoto kwa familia nyingi Guatemala na kuwafanya wazazi kushindwa kuwapeleka shule watoto bila kuwa na uhakika wa mlo.

Minogni mwa wanufaika wa mradi huo unaofadhiliwa na FAO ni msichana Dulce María Díaz Pérez mwenye umri wa miaka 12 ambaye hutamani sana kusoma vitabu.

“Nafurahia shamba la shule yetu na ningipenda kila shule iwe shamba kama hili”, Asema  Diez.

Naye Dulce, mwanfunzi wa daraja la sita kwenye shule ya Tejutla, San Marcos, eno la Western Highlands Maghahribi ya Guatemala, anajufunza kuhusu kilimo endelevu katika shamba lilo pia kwenye eneo la shule yao.

Shambani ndiko tunapata fursa ya kujifunza mengi mno, asema Dulce.

Shamba la shule la Dulce nchini Guanteamala ni sehemu ya juhudi nyeti za taifa kuhakikisha lishe mashuelni ambao umesaidia kuziunganisha shule, familia na jamii kwa ujumla. Baada ya mradi huo kuanza kwa majaribio sasa FAO inasema shule Mfano wa kuigwa wa shule hilo ni ule unaoendeshwa na FAO nchini Brazil ambao ndio ilikuwa chachu ya kuanzishwa mradi wa Guatemala mwaka 2014. 

Juhudi hizi zimeshabikiwa na kuwezeshwa azaidi na serikali, jamii, mashirika na kukumbatiwa na wazazi, shule na wanafunzi wenyewe na sasa umeweka historia ya masuala ya chakula mashuleni Guatemala ambayo shule nyingi zimeanza kuitekeleza mwaka 2018 bada ya hatua za kutokomeza njaa kupitishwa na bunge nchini humo likishirikiana na FAO.

FAO inasema mradi huu wa chalula mashuleni mbali ya kuhamasisha Watoto wengi kuhudhuria shule unalenga kuboresha pia afya lakoini pia  kuhakikisha kwamba mazao ya kilimo ya wenyeji yanapata soko.