Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake kutokuwa na sauti kunachochea ndoa za utotoni na ukeketaji Kajiado, Kenya- Bi. Parit

Dorcus Parit, mwanzilishi na mkurugenzi wa kituo kinachowahifadhi wasichana walioko hatarini ya ndoa za utotoni na ukeketaji kaunti ya Kajiado nchini Kenya.
UNnewskiswahili/Patrick Newman
Dorcus Parit, mwanzilishi na mkurugenzi wa kituo kinachowahifadhi wasichana walioko hatarini ya ndoa za utotoni na ukeketaji kaunti ya Kajiado nchini Kenya.

Wanawake kutokuwa na sauti kunachochea ndoa za utotoni na ukeketaji Kajiado, Kenya- Bi. Parit

Wanawake

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake kikao cha 63 unaendelea hapa New York, Marekani ambapo vikao mbali mbali vinafanyika katika kupaza sauti za wanawake na kujadili changamoto wanazokabiliana nazo lakini pia jinsi ya kuzitatua.

Suala la ndoa za utotoni ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazozikabili jamii nyingi  na huku Umoja wa Mataifa usisitiza tatizo hilo lililomea mizizi na kuwa kama donda ndungu lazima likomeshwe kabla ya mwaka 2030. Hivi sasa serikali, jamii na hata wanaharakati wameamua kulivalia njuga suala hilo . Mmoja wa wanaharakati hao ni mwanamke Dorcus Parit mwanzilishi na mkurugenzi wa  kituo cha mpito cha Hope Beyond huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambacho ni kimbilio kwa wasichana wanaoingizwa kwenye ndoa za utotoni au wale wanaokabiliwa na hatari ya kukeketwa.  

Kandoni mwa mkutano huo wa CSW63 Bi Parit amesema idadi ya wasichana wanaokabiliwa na hali hii ni wengi huku akitoa mfano.

(Sauti ya Parit)

Halikadhalika amelalamikia kwamba bado wanawake wanakandamizwa na hivyo

(Sauti ya Parit)