Kuna hatua katika kupambana na unyanyasaji na ukatili wa kingono UN

18 Machi 2019

Umoja wa Mataifa umeorodhesha visa 259 vya madai ya unyanyasaji na ukatili wa kingono (SEA) mwaka 2018 kwa mujibu wa ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres iliyowasilishwa leo kwenye Baraza JKuu la Umoja huo. Ingawa idadi ya visa imeongezeka ikilinganishwa na miaka miwli iliyopita , ripoti inaonyesha ongezeko la uelewa miongoni mwa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wanaohusiana na Umoja wa Mataifa , na kumekuwa na nyenzo zilizoboreshwa za kutoa tarifa katika mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa.

Unyanyasaji wa kingoni “ni ukatili au jaribio la ukatili wa kutumia upenyo wa nafasi, tofauti za madaraka, au uaminifu kwa asili ya faida za kingono ikiwa ni pamoja na kujipatia fedha, fursa za kijamii au kisiasa kutokana na unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwingine”

Kwa upande wau moja wa Mataifa ukatili wa kingono ni “kitendo halisi au tishio la kimwili lenye mwelekeo wa kingono , iwe kwa shuruti au kwa mazingira yasiyo na uwiano.”

Kwa mujibu wa ripoti hiyo hadi sasa sio madai yote ambayo yamehakikiwa na mengi bado yanafanyiwa uchunguzi au bado yako katika tathimini za awali.

Uhalisia katika idadi

Kuanzia tarehe Mosi Januari hadi tarehe 31 Disemba 2018 , Umoja wa Mataifa ulipokea jumla ya madai ya SEA 148 yanayohusisha moja kwa moja  wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa , 111 kutoka mashirika wadau yanayoendesha program za Umoja wa Mataifa. Hii inadhihirisha ongezeko la matukio ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo madai yanyowasilishwa yalikuwa jumla 138, na mwaka 2016 ambayo yalikuwa jumla ya madai 165.

Hata hivyo ripoti inasema katiia operesheni za ulinzi wa amani dalili zinatia moyo kwa visa kupungua karibu kwa nusu katika miaka miwili iliyopita, wakati visa 103 viliripotiwa mwaka 2016 mwaka 2018 madai yaliyowasilishwa ni 54 pekee.

Vingi vya visa vilivyowasilishwa mwaka jana vinahusisha mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya afrika ya Kati CAR, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wa MONUSCO, nchini Mali MINUSMA, nchini Haiti MINUSTAH, Liberia UNMIL na Sudan Kusini UNMISS. Na hakuna madai yoyote yaliyowasilishwa dhidi ya operesheni maalum za kisiasa za Umoja wa Mataifa.

Licha ya hatua kubwa zilizopigwa kuboresha hali katika operesheni za ulinzi wa amani , bado idadi ya madai imeenda juu dhidi ya wafanyakazi wa mashirika ya UN, ambapo mwaka 2018 yameongezrka na kufikia 94 ukilinganisha na 50 ya mwaka 2017.

Ripoti inafafanmua kuwa kibaya zaidi ni kwamba idadi ya madai dhidi ya mashiririka wadau wanaotekeleza programu za Umoja wa Mataifa yamepanda na kufikia  109 ongezeko la Zaidi ya robo ikilinganishwa na madai 25 tu yaliyowasilishwa mwaka 2017.

Na kwa kuongezea madai mawili mengine yaliripotiwa 2018 dhidi ya vikosi ambavyo si vya Umoja wa Mataifa ambavyo vimeidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wakati 2017 ilikuwa ni dai moja na 2016 dai moja.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo idadi inaonyesha kwamba “ mtazamo wa kujikita Zaidi na waathirika uliochukuliwa na Umoja wa Mataifa na kuanza kutekelezwa mwaka mmoja uliopita unaleta tija kwani inaonekana kuwepo na ongezeko la kuwa na Imani miongoni mwa waathirika na manusura kujitokeza na kutoa taarifa.”

PICHA: UN/Nektarios Markogiannis
Vitu vya kuchagiza kupambana na unukatili na unyanyasaji wa kingono vikihimiza "hakuna uvumilivu , hakuna sababu" katika mtazamo wa SEA kwa wafanyakazi wa umoja wa Mataifa

Juhudi zinazofanywa na UN sasa na kuelekea mbele

Mkakati wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika awamu ya kwanza unajikita katika kushughulikia masuala katika mfumo wa Umoja wa Mataifa pamoja na ya wale ambao wameidhinishwa na Umoja wa Mataifa kuendesha programu mbalimbali. Idadi yake ni zaidi ya wafanyakazi 90,000 katika zaidi ya mashirika na vyombo 30 na kujumuisha walinda amani 100,000. Miradi mbalimbali imeanzishwa hadi sasa ikiwemo

. utoaji ripoti kila robo mwaka ambayo ni ya wazi kuhusu suala la SEA

. Kuteuliwa kwa mwakilishi wa kimataifa wa haki za waathirika , hali kandhalika wengine wengi huko mashinani.

. Kuzinduliwa Septemba mwaka jana “mzunguko wa uongozi” ukihusisha viongozi wa dunia wakiahidi kukomesha SEA kwenye mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa.

. Kuweka mfumo wa kufuatilia msaada kwa waathirika ili kuhakikisha kwamba huduma zinatolewa kwa manusura na waathirika ipasavyo na kwa mpangilio.

. Na kuzinduliwa mwezi Oktoba kwa nyenzo ya kielektroniki iitwayo “ukaguzi wa wazi” wa kuwachunguza wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliofutwa kazi kwa sababu ya madai ya unyanyasaji na ukatili wa kingono, au wale waliojiuzulu au waliositishwa wakati uchunguzi ukifanyika.

Suala la uwajibikaji

Kwa kuwa Umoja wa Mataifa hauna mamlaka au uwezo wa kisheria wa kuwafungulia watu mashitaka , uwajibikaji wa uhali wa watu binafasi unaendelea kuwa mikononi mwa nchi husika. Katika visa ambapo anayedaiwa kutekeleza SEA ni raia , umoja wa Mataifa unafanya uchunguzi wa kiutawala , mfanyakazi anatimuliwa wakati madai yanapohakikiwa na endapo Umoja wa Mataifa utathibitisha kuwa uhalifu ulitendeka unapeleka kesi hiyo kwa mamlaka ya nchi husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

Wakati kesi zinahusisha walinda amani, nchi wachangiaji vikosi zina mamlaka mahsusi ya kuchunguza, lakini Umoja wa Mataifa utashirikiana kwa karibu nan chi hiyo kuchapuza uchunguzi na kufuatilia kwa kuzingatia suala la uwajibikaji.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud