Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres aelezea kusikitishwa na vifo kutokana majanga Indonesia huku akitoa mshikamano kwa mamlaka.

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres
UN /Manuel Elias
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres

Guterres aelezea kusikitishwa na vifo kutokana majanga Indonesia huku akitoa mshikamano kwa mamlaka.

Msaada wa Kibinadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea kusikitishwa kwake na vifo, uharibifu wa mali na kufurushwa kwa watu kufuatia mafuriko na tetemeko la ardhi huko Sentani, Jayapura na Papua magharibi mwa jimbo la Tenggara nchini Indonesia.

Bwana Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake ametoa salamu za rambirambi kwa familia na waathirika na kwa watu na serikali ya Indonesia.

Halikadhalika Umoja wa Mataifa umeelezea mshikamano na mamlaka Indonesia na kuelezea utayari wa Umoja huo kufanya kazi nao wakati huu wakijibu mahitaji ya kibinadamu yanayotokana na majanga mawili hayo ya asili.

 

TAGS: Antonio Guterres, Indonesia, tetemeko la ardhi.