Mchango wa wanawake katika amani ya kudumu Kenya ni dhahiri-Embrace

18 Machi 2019

Mkutano wa 63 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW63 umeingia siku ya sita hii leo Jumatatu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambako kunafanyika mikutano kando ikiratibiwa na nchi wanachama ili kuonyesha kwa kina kile inachofanya mashinani kumnasua mwanamke.

Moja wa mikutano hiyo ya kando ni ule ulioangazia uongozi wa wanawake katika kuelekeza kujenga utamaduni wa amani kwa ajili ya jamii endelevu ukisimamiwa na Kenya na Indonesia chini ya uwezeshaji wa Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ili kuwepo amani ya kudumu, sauti za wanawake zinahitajika, kuanzia kuzuia, kusuluhisha mizozo na kuleta uwiano na kuimarisha uchumi baada ya mizozo na kwamba ushiriki wa wanawake kikamilifu unaimarisha fursa za makubaliano ya amani kudumu.

Ni kwa kuendana na dhamira hiyo ndipo wanawake wenye ushawishi nchini Kenya wamechukua jukumu la kuchagiza amani na kuanzisha kikundi cha kusongesha harakati za kuleta amani kwa jina la Embrace. 

Mmoja wa wanawake hao, Bi Ida Odinga ambaye ni mwenyekiti wa kundi hilo pindi tu baada ya mkutano wao amezungumza na Idhaa ya Kiswahili ambapo amesema

Sauti ya Ida

Kwa upande wake bi Rachel Shebesh katibu tawala kwenye wizara ya maswala ya jinsia, wazee na watoto Kenya na mwanachama wa Embrace amesema lengo na kundi hilo ni pamoja na

Sauti ya Shebesh

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter