Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viwango vipya vya kimataifa vyaweka kupambana na tatizo la mihadarati:UN

Mtumiaji wa mihadarati akitumia dawa  mbadala kwa ajili ya kuondowa hamu ya mihadarati
Picha/IRIN/Sean Kimmons
Mtumiaji wa mihadarati akitumia dawa mbadala kwa ajili ya kuondowa hamu ya mihadarati

Viwango vipya vya kimataifa vyaweka kupambana na tatizo la mihadarati:UN

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Muungano wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wataalam wa haki za binadamu wanaokutana kwa ajili ya mkutano wa tume ya masuala ya madawa ya kulevya mjini Vienna Australia, leo umezindua viwango vipya vya kimataifa vya kisheria ili kuandaa na kubadili mtazamo wa vita vya kimataifa dhidi ya tatizo la mihadarati.

Viwango hivyo vya kimataifa vya muongozo kuhusu haki za binadamu na sera za mihadarati vinaaninisha viwango vya haki za binadamu katika vita hivyo. Kwa kutumia miongo ya ushahidi , vinatoa mwongozo kwa serikali ili kuunda sera za madawa ya kulevya zinazoingatia haki za binadamu, zikigusa maeneo yote kuanzia uzalishaji hadi matumizi.

Pia kwa kukumbatia muundo wa haki za binadamu duniani mwongozo huo unagusa maeneo mengi ya sera kuanzia za maendeleo, mfumo wa haki za sheria hadi afya ya jamii.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa udhibiti wa mihadarati unaenda sanjari na utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu CDGs ya mwaka 2030 na nchi wanachama zimeahidi kutomuacha yeyote nyuma . Kwa kuzingatia ajenda hiyo ya 2030 mkakati wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP wa mwaka 2018-2-021 na wa HIV, afya na mkakati wa maendeleo wa 201602021 : vinaunganisha mambo haya maiwli na “mwongozo wa kimataifa kuhusu haki za binadamu na sera za mihadarati, unatoa viwango vya kimataifa vya kisheria ambavyo vinaweka utu wa mt una maendeleo endelevu katika kitovu cha hatua za nchi wanachama kukabiliana na uchumi haramu wa mihadarati.

Muongozo huo mpya umeandaliwa na muungano wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, shirika la afya ulimwenguni WHO, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS, UNDP, wataalam wa haki za binadamu na wataalam wa sera za mihadarati.

Muongozo huo ni mfano wa msaada unaotolewa na UNDP katika kutoa katika kuzijumuisha ahadi za kimataifa za haki za binadamu mipango na sera kitaifa, kikanda na kimataifa. UNDP inasema muongozo huu umekuja wakati muafaka ambapo kuna Ushahidi tosha wa kushiondwa kwa mifumo iliyopo ikiwemo kukita mizizi kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na hivyo serikali ziknaombwa kubadili mmwelekeo.