Msaada wa kwanza wa WFP wawafikia waathirika wa kimbunga Msumbiji

15 Machi 2019

Kimbunga IDAI kimeukumba mji wa bandari wa Beira ulio na wakazi wengi nchini Msumbiji ,na kusababisha mafuriko makubwa ambayo yameshaathiri maeneo mengine Kusini mwa Afrika ikiwemo Kusini mwa Malawi na Mashariki mwa Zimbabwe. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP limekuwa likiongeza juhudi zake za maandalizi ili kukidhi mahitaji ya misaada inayohitajika kwa waathirika. Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo Herve Verhoosel

(SAUTI YA HERVE VERHOOSEL)

“Watu zaidi ya 900.000 nchini Malawi na 600,000 nchini Msumbiji wameathirika na mafuriko wiki hii yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoambatana na mfumo wa kimbunga, maisha ya watu wengi yamepotea, wengine kwa maelfu wametawanywa na nyumba , barabara, madaraja na mazao vimesambaratishwa.”

Ameongeza kuwa hivi sasa serikali za Malawi na Msumbiji zimetangaza hali ya dharura katika maeneo yaliyoathirika na zimeomba msaada kutoka nje.

Wafanyakazi wa WFP wamekuwa wakifanya tathimin I ili kubaini kiwango cha uharibifu kilichosababishwa na mafuriko hayo hadi sasa na kutoa kipaumbele cha mahitaji.Shirika hilo linasema tathimini ya ziada ni muhimu wakati kimbunga kikiendelea. Hatua hii ya pili ya tathimini imekuwa ngumu linasema shirika la WFP kwa sababu ya ukweli kwamba maporomoko ya udongo yanachangia, mifumo ya mawasiliano imezidiwa na safari za anga nchini Msumbiji zimesitishwa hivi sasa kutokana na hali mbaya ya hewa. Mbali ya helkopta ambazo zimeshatumwa na serikaliya Afrika Kusini , WFP itapeleka takribani helkopta moja hali ya anga ikiruhusu  kwa ajili ya operesni za dharura za anga nchini Msumbiji maeneo ya vijijini ambayo yanauwezekano mkubwa wa kutokuwa na njia ya mawalsiliano kabisa kutokana na mafuriko. Msemaji wa WFO amesema hadi kufikia sasa

((SAUTI YA HERVE VERHOOSEL)

“Akiba ya chakula katika nchi zilizoathirika na kwingineko Kusini mwa Afrika kama vile nchini Afrika Kusini na Zambia na hicho kinaweza kusaidia katika hali hii”

Pia ameongeza kuwa biskuti za kuongeza nguvu zimesafirishwa kwa ndege hadi Beira kutoka kwenye kituo cha dharura cha WFP kilichopo Dubai na zitawasili kesho Machi 16.

WFP imepeleka wafanyakazi wa ziada katika maeneo athirikaikiwemo Malawi na inatumia kila njia ikiwemo ndege zisizo na rubani au drines kubaini mahitaji na kuyashughulikia cha msingi kinachohitajika kwa sasa ni fedha za ufadhili ili kuendelea kutoa msaada limesema shirika hilo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud