Mazingira wanayoishi Wasyria yanasikitisha , UN yahitaji dola bilioni 8.8 kuwanusuru.

Raia wa Roma wakiwa njiani kutafuta mahali salama Kosovo.
UNHCR/Roger LeMoyne
Raia wa Roma wakiwa njiani kutafuta mahali salama Kosovo.

Mazingira wanayoishi Wasyria yanasikitisha , UN yahitaji dola bilioni 8.8 kuwanusuru.

Msaada wa Kibinadamu

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola bilioni 8.8 kwa ajili ya kuwasaidia mamilioni ya Wasyria wanoishi katika mazingira magumu nje na ndani ya nchi hiyo iliyoghubikwa na machafuko pamoja na jamii zinazowahifadhi.

Miaka minane tangu kuanza kwa mgogoro, kuna Wasyria milioni 12 wakimbizi ama wakimbizi wa ndani idadi ambayo ni karibu nusu ya watu wote kabla ya kuzuka vita.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa machafuko yamepungua katika miezi ya hizi karibuni lakini, mabomu yanaendelea kumiminika kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Tume huru ya kimataifa ya uchunguzi kuhusu Syria, Paulo Pinheiro iliyotolewa Jumanne wakati kukishuhudia mashambulizi ya angani magharibi mwa jimbo la Idlib na huku kukiwa na ripoti kuwa ISIL wanakaribia kushindwa Mashariki mwa Syria.

Chaguo gumu kwa familia zilizofurushwa

Takriban asilimia 70 ya wakimbizi kutoka Syria wanaishi katika mazingira magumu na katika hali ya umaskini kwa mujibu wa kamishna mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi ambaye ametembelea Syria na Lebanon hivi majuzi ambako wakimbizi ni robo ya wakazi wote nchini Lebanon.

Bwana Grandi amesema upungufu wa msaada wa fedha umesababisha ukata na kupelekea wakimbizi kusalia na chaguo gumu kila siku kama vile kuwaondoa watoto shule ili wafanye kazi na kupunguza ugumu wa maisha.

Ndani ya ombi hilo dola bilioni 3.3 zinahitajika kwa ajili ya msaada ndani ya Syria na bilioni 5.5 kwa ajili ya kusaidia jamii zinazowahifadhi pamoja na nchi jirani.

Akitoa anaglizo kwamba mzozo haujamalizika, mkuu wa ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA, Mark Lowcock amesema bila msaada wa fedha misaada ya dharura na ya kuokoa maisha itaathriwa vibaya. Akisisitiza kwamba, “kila mwanamke, mwanamume, mtoto wa kike na kiume nchini Syria ambaye anahitaji msaada wetu anapaswa kuupata.”

Kwa upande wake mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, Achim Steiner ameonya kuhusu jamii na viwango vya juu vya umaskini Syria na umuhimu wa kusaidia jamii zinazowahifadhi wakimbizi pia.

Shuleni mjini Aleppo Syria, wanafunzi wanafundishwa namna ya kutembea kwa usalama. Miongoni mwa wanayoambiwa ni pamoja na kuepuka kupita katika njia nyembamba au vitu katikati ya barabara vinavyoweza kugharimu maisha yao.
UNICEF/Grove Hermansen
Shuleni mjini Aleppo Syria, wanafunzi wanafundishwa namna ya kutembea kwa usalama. Miongoni mwa wanayoambiwa ni pamoja na kuepuka kupita katika njia nyembamba au vitu katikati ya barabara vinavyoweza kugharimu maisha yao.

 

 Baraza la haki za binadamu limeelezwa kuhusu mabomu kurushwa

Akihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa bwana Pinheiro amesema kuwa kuna idadi kubwa ya Wasyria wanaohaha kukimbia machafuko. Akiongeza kuwa, “mabomu yanaendelea kusikika na raia wanabeba gharam kubwa na maisha yao huku uhasama unaoshuhudiwa ukihatarisha maisha yao na mbinu za kujipatia kipato kwa wale wanaotoa kauli ya kurejea nyumbani.”

Bwan Pinheiro amesisitiza kwamba mzozo ambao kwa sasa umeingia mwaka wa tisa unaendelea kuleta zahma kwa maelfu ya raia na wakimbizi wa ndani wanaendela kukabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo katika maeneo yaliyonyakuliwa na serikali.

“Kunyanyapaliwa, ubaguzi na mateso mengine vinaendelea kushuhudiwa Idlib, Douma, Dara’a na kaskazini mwa Hom,” amesema Pinheiro. Ameongeza kuwa, kushikiliwa kiholela, na kuzuiliwa katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali ikiwemo Mashariki mwa Ghouta, Dara’a na kaskazini mwa Hom kunaendelea kushuhudiwa.

Aidha mauji na vifo vizuizini vinaendelea amesema Pinheiro akielezea mahakama zisizo na utaratibu zinazoendeshwa na serikali ya Syria ikiwemo mifumo inayobuniwa ya sheria ya vikundi vilivyojihami na vikundi vya kigaidi.

Katika kujibu madai hayo ujumbe wa Syria umelalamikia kile mazingira ya siasai na kusisitiza kuwa serikali yake inajaribu kulinda raia wake kutokana na ugaidi.