Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubunifu pekee ndio utakaotufikisha katika mtakabali tunaoutaka:UNEA

Dau la kijadi lenye urefu wa mita 9 lilolotengenezwa kwa tani 10 za mabaki ya plastiki, ni dau la kwanza la aina yake kuzinduliwa likionyesha ubunifu wa kukabiliana na changamoto za mazingira
UN Environment

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kwa kutumia ubunifu pekee ndio daraja la kizazi hiki kuweza kuipeleka dunia karibu na mtazamo ulioainishwa kwenye  mustakabali tunaoutaka kwa ajili ya wote ifikapo mwaka 2030. 

Kauli hiyo imeelezwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEA linaloendelea jijini Nairobi nchini Kenya. Mkutano huo wa nne wa Baraza kuu la mazingira uliojikita katika kaulimbiu” “Suluhu bunifu kwa changamoto za mazingira na uzalishaji na matumizi endelevu” unajadili mbinu mbadala za kukabiliana nachangamoto za mazingira huku ikihakikishwa kwamba hakuna anayesalia nyuma katika kutimiz aajenda ya maendeleo endelevu yamwaka 2030 hasa katika malengo ya husuyomazingira ikiwemo nchi kavu na baharini.

Kwa mujibu wa UNEA mambo muhimu ya kufikia lengo hilo la njia mbadala ni kuendeleza na kuchagiza utamaduni wa ubunifu, uwazi na ushiriki.

Na utamaduni wa ubunifu utapaswa kugusa sekta zote  na wadau wote ili kuhakikisha wanapata haki zao za ushiriki, jambo ambalo UNEA linasema litasaidia katika kutokomeza umasikini, kubadili mtazamo kutoka uzalishaji na matumizi yasiyoendelevu kuyingia katika matumizi endelevu, na kulinda na kudhibiti mali asili.

UNEA imesisitiza masuala ya muhimu yanayohitajika kuhakikisha uchagizaji na uimarishaji wa utamaduni wa ubunifu. Masuala hayo niuongoz, taasisi za utawala zinazokumbatia ubunifu, uwazi na ushirikiano, elimu na kuzijengeaja uwezo ili kuhamisha ujuzi kutoka kwa wachache kwenda kwa jamii na kutenga fungu maalumu la fedha na tekinolojia kuhakikisha mchakato huu unakuwa endelevu.

Baraza hilo la nne la mazingira lilianza Jumatatu Machi 11 na litakamilika Ijumaahii Machi 15 linahimiza maeneo matatu muhimu ambayo washiriki wanaenda kuyafanyia kazi katika nchi zao.

Mkaa unaotokana na miti unachangia katika uharibifu wa mazingira lakini sasa ukwajukwaju watumika huko Ethiopia kuandaa mkaa
FAO/Giulio Napolitano
Mkaa unaotokana na miti unachangia katika uharibifu wa mazingira lakini sasa ukwajukwaju watumika huko Ethiopia kuandaa mkaa

Maeneo hayo ni changamoto za mazingira zinazohusiana na umasikini na udhibiti wa maliasili ikiwemo mifumo endelevu ya chakula, uhakika wa chakula na kuzuia kupotea kwa bayoanuai, pili ni matumizi bora ya rasilimali, nishati, madawa, na udhibiti wa taka na tatu biashara bunifu ambazo zina mnepo hasa katika wakati huu ambapo kuna mabadiliko makubwa ya teknolojia.

Kauli hiyo imeelezwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEA linaloendelea jijini Nairobi nchini Kenya. Mkutano huo wa nne wa Baraza kuu la mazingira uliojikita katika kaulimbiu” “Suluhu bunifu kwa changamoto za mazingira na uzalishaji na matumizi endelevu” unajadili mbinu mbadala za kukabiliana nachangamoto za mazingira huku ikihakikishwa kwamba hakuna anayesalia nyuma katika kutimiz aajenda ya maendeleo endelevu yamwaka 2030 hasa katika malengo ya husuyomazingira ikiwemo nchi kavu na baharini.

Kwa mujibu wa UNEA mambo muhimu ya kufikia lengo hilo la njia mbadala ni kuendeleza na kuchagiza utamaduni wa ubunifu, uwazi na ushiriki.

Na utamaduni wa ubunifu utapaswa kugusa sekta zote  na wadau wote ili kuhakikisha wanapata haki zao za ushiriki, jambo ambalo UNEA linasema litasaidia katika kutokomeza umasikini, kubadili mtazamo kutoka uzalishaji na matumizi yasiyoendelevu kuyingia katika matumizi endelevu, na kulinda na kudhibiti mali asili.

Kituo cha maji cha Abu Shouk katika kambi ya wakimbizi wa ndani, Darfur, Sudan ambako vita vinaathiri mazingira.
UNAMID/Albert González Farran