Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tukaze mkanda asilimia 7 tu ya wanawake ndio viongozi wa nchi:UN

Kikao cha kamisheni ya hali ya wanawake kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa
UN Photo/Loey Filipe.
Kikao cha kamisheni ya hali ya wanawake kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Lazima tukaze mkanda asilimia 7 tu ya wanawake ndio viongozi wa nchi:UN

Wanawake

Usawa wa kijinsia bado ni changamoto kubwa duniani na ni jukumu la kila mtu kuhakikisha wanawake wanapata fursa na usawa unaostahili kwa vitendo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa ufunguzi wa kikao cha 63 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani kilichoanza leo.

Akihimiza umuhimu wa kuhakikisha mwanamke anapata usawa katika ngazi zote kwenye jamii kuanzia utawala na hata kujikwamua kiuchumi Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa mabadiliko na kubadili mwelekeo kwani sio hali ya wanawake tu bali hali ya uongozi kwa wanawake  na kuongeza kwamba.

Mwanamke amekuwa akikandamizwa kwa muda mrefu kutokana na mfumo dume uliotawala lakini hilo sasa halina nafasi

Usawa wa kijinsia kimsingi ni suala la madaraka, kwa karne wanawake wamekuwa waki tenga kwa maksudi, kupuuzwa, na kunyamazishwa katika dunia ambayo inatawaliwa na wanaumme na utamaduni wa mfumo dume.”

Ameongeza kuwa “Leo hii hebu tuwe wazi kuhusu haja ya mabadiliko , endapo wanawake hawatochukuliwa kuwa ndani ya mfumo wa madaraka , kwa hakika ni madaraka ndio tunayohitaji kutafafanua bayana na sio wanawake. Tunawahitaji na tunawahitaji sasa , na kuliko wakati mwingine wowote kwani dunia yetu imepotea bila nyinyi.”

 Amesisitiza kwamba dunia hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingo kuanzia mabadiliko ya tabia nchi migawanyiko katika jamii , kutokuwepo usawa , ukosefu wa usalama na mengineyo na mshikamano wa kimataifa unakabiliwa na msukosuko mkubwa katika kutatua changamoto hizo.

Kana kwamba hayo hayatoshi duniani kote kumekuwa na ongezeko la shinikizo katika haki za mwanamke  na kwamba “ shinikizo hilo ni kubwa lisilojali na la kuumiza, tunashuhudia ukatili dhidi ya wanawake, hususan watetezi wa haki za binadamu na wanawake wanaoshiriki vinyan’ganyiro vya uongozi wa kisiasa.”

 Hata hivyo licha ya changamoto hizo amewataka wanawake kuendelea kuwa jasiri kupugania haki zao na kuhakikisha dunia inatambua mchango wao.

“Sote tunajua kwamba ushiriki wa wanawake unaleta mabadiliko katika mikataba ya amani na inakuwa ya kudumu zaidi , lakini bado tunachangamoto ya kuhakikisha wanajumuishwa katika timu za majadiliano na hata katika uongozi w anchi ni asilimia 7 tu ya wanawake ndio wanaoshika wadhifa huo na hata nchi ambazo zinapaza sauti kuunga mkono ajenda hii bado zinashindwa kutekeleza kwa vitendo kauali zao pale inapohitajika.”

Mkutano huu ambao umewaleta pamoja zaidi ya washiriki 9000 kutoka wawakilishi wa nchi 193 wanachama wa umoja huo pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale ya kiraia kujadili jinmsi gani mwanamke ataweza kukombolewa katika suala zima la uongozi lakini vilevile kumpatia mwanamke uwezo wa kuongeza mchango wake katika jamii.

Ameongeza kuwa sasa wakati umefika wa kuhakikisha hilo linapingwa, linatoikomezwa na halikubakiki katika kila jamii.

Katika mkutano huu, ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Waziri wa afya Ummie Mwalimu ambapo mratibu wa ujumbe huo, Profesa Linda Mhando amesema Tanzania itakuwa na matukio ya kando yakilenga maudhui makuu  ya mkutano huo.

(Sauti ya Profesa Linda Mhando)

 Matukio hayo ni miundombinu endelevu kwa usawa wa jinsia siku ya jumanne, mifumo ya Ulinzi wa Jamii siku ya jumatano na uwezeshaji wanawake na wasichana tarehe 20 ya wiki ijayo