Hatua za Benki ya Dunia dhidi ya Ebola DRC zazaa matunda

11 Machi 2019

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC harakati zinaendelea ili kutokomeza mlipuko wa Ebola unaoelezwa kuwa ni wa pili kwa ukubwa kuwahi kukumba taifa hilo la Maziwa Makuu.Benki ya Dunia inasaidia sambamba na manusura wa ugonjwa huo wako mstari wa mbele kama anavyosimulia Grace Kaneiya.

Sauti hiyo ya Masika Lubaho, mama wa watoto watano akizungumza wakati akiingia kwenye kituo cha kutibu wagonjwa wa Ebola, kilichoko mji wa Beni, jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC.

Katika kituo hiki kinachoendeshwa na shirika la kiraia la ALIMA, binti yake Masika amefungiwa katika chumba maalum wakizungumza kupitia turubai. Masika anasema..

(Sauti ya Masika Lubaho)

Wagonjwa waliothibitishwa kuwa na Ebola wanawekwa kwenye chumba maalum kwa ajili ya matibabu, chumba ambacho ni rahisi kwa wahudumu wa afya kumuona mgonjwa au kuzungumza naye hata wakiwa nje.

Ukata katika huduma za afya ulikuwa ni moja ya vikwazo vya kukabiliana na Ebola lakini Benki ya Dunia imechangia zaidi ya asilimia 50 ya operesheni dhidi ya ugonjwa huo nchini DRC na kutoa fedha za ruzuku ili kuhakikisha huduma za afya dhidi ya Ebola ni bure.

Hata hivyo kwa wakazi wengine wa Beni kama Kasomo Kavira simulizi ni chungu..

(Sauti ya Kasomo Kavira)

Hata hivyo baada ya yeyé kupona Ebola…

(Sauti ya Kasomo Kavira)

Mlipuko wa sasa wa Ebola huko DRC uliotangazwa Agosti Mosi mwaka 2018, ni wa pili kwa ukubwa zaidi kwenye historia ya Ebola nchini humo ambapo hadi sasa kati ya wagonjwa takribani 900 walioripotiwa, zaidi ya 560 wamefariki dunia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud