Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubia mpya wa FAO na GAIN kuboresha lishe kwa masikini

Maziwa yana uwezo wa kuboresha lishe kwa familia za wafugaji
Picha EADD/Neil Thomas/FAO
Maziwa yana uwezo wa kuboresha lishe kwa familia za wafugaji

Ubia mpya wa FAO na GAIN kuboresha lishe kwa masikini

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na muungano wa kimataifa wa kuimarisha lishe GAIN wamekubaliana kuungana katika kuongeza upatikanaji na urahisi wa chakula chenye lishe kwa ajili ya wote kwenye nchi zinazoendelea.

Kwa mujibu wa FAO ushirika wao ulitiwa saini jana Alhamisi kwa lengo la kuwezesha mifumo jumuishi ya kilimo na mifumo ya chakula ikijikita katika mitazamo mipya ambayo itahusisha makampuni madogo yay a wastani (SMEs) kuchagiza suluhu za soko kama nyenzo muhimu ya kuboresha lishe.

FAO na GAIN pia watashirikiana kuweka mifumo ya vyakula mijini  kuzingatia Zaidi lishe bora , kwa kupitia msaada wa mpango wa GAIN wa udhibiti wa lishe mijini na ajenda ya FAO ya vyakula mijini.

FAO inasema hivi sasa Zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wanaishi mijini na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 70 ifikapo mwaka 2050, na hii inaleta changamoto kubwa katika uzalishaji na usambazaji wa chakula.

Shirika hilo limeongeza kuwa uhakika wa chakula na lishe kwa watu masikini mijini bado ni hatari kubwa kutokana na kupanda kwa gharama na mfumoko wa bei za vyakula, majanga ya asili na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akikumbusha kuhusu azimio la hivi karibuni la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ‘afya ya kimataifa na seraza nje:dunia bora kupitia lishe bora” mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva ametoa wito wa kushikama kuchagiza lishe bora akisema “Ni lazima tutoe msukumo Zaidi katika kuchagiza lishe bora hususan sasa ambako utipwatipwa umekita mizizi. Tunafahamu chanzo kikuu cha njaa na jinsi ya kuikabili lkini bado kuna haja ya ufuatiliaji mkubwa na wa kila mara ili kufanya mifumo ya chkula kuwa salama na yenye mnepo na sekta binafsi zina jukumu kubwa katika hili , bila wao hatuwezi kusonga mbele na ajenda hii.”

Mkurugenzi huyo ameongeza kwamba lishe bora ni muhimu katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu au SDGs, na hili linahitaji hatua ili kuwezesha mifumo ya chakula kufikisha lishe ya gharama nafuu kwa wote.

Amesema FAO inashika usukani katika safari hii imefurahi kuimarisha ushirikiano na GAIN leo hii ili waweze kujikita katika kuzisaidia kampuni za biashara na serikali kuhakikisha zinafikisha lishe bora kwa watu wake.

Graziano amesema kujenga mnepo wa mifumo ya chakula kwa ajili yah apo baadaye kwa kujumuisha maeneo ya vijijini na mijini , na kuimarisha uwiano uliopo kwa kuhusisha wadau wote kutawafaidisha wakulima wadogowadogo na watu masikini mijini.