Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pengo la usawa wa kijinsia kwenye ajira bado halijazibwa-ILO

Profesa Amivi Kafui Tete-Benissan (kushoto) ambaye anafundisha biolojia na kemia kwenye chuo kikuu cha Lomé, Togo, pia ni mwanaharakati ambaye anachagiza wasichana kushirika kazi za sayansi.
World Bank/Stephan Gladieu
Profesa Amivi Kafui Tete-Benissan (kushoto) ambaye anafundisha biolojia na kemia kwenye chuo kikuu cha Lomé, Togo, pia ni mwanaharakati ambaye anachagiza wasichana kushirika kazi za sayansi.

Pengo la usawa wa kijinsia kwenye ajira bado halijazibwa-ILO

Wanawake

Hatua katika kuziba pengo la usawa wa kijinsia zimekwama, na katika baadhi ya sehemu zinarudi nyuma, imesema ripoti ya shirika la kazi ulimwenguni, ILO kuhusu mtazamo wa wanawake kwenye sekta ya ajira ya mwaka 2018, ripoti ambayo imetolewa leo Alhamisi.

ILO imesema pengo la usawa wa kijinsia kwa mujibu wa soko la ajira halijapungua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita hali ambayo inaleta wasiwasi.

Imesema ijapokuwa mwenendo uliopo unabadilika, na sera ambazo zinajali usawa wa kijinsia zizingatiwe hali inatarajiwa kudorora zaidi wakati mifumo ya kazi inabadilika na mustakabali wa baadaye hautabiriki.

Kuziba pengo la usawa wa kijnisia

Ripoti inasema kuwa dhana ya kwamba pengo la usawa wa kijinsia ni kwa sababu wanawake hawataki kufanya kazi nje ya myumbani sio kweli kwani katika asilimia 70 ya wanawake waliohojiwa walisema wangependela kuwa katika kazi zinazolipa huku asilimia 66.5 wakikubaliana na hilo hata hivyo mwaka 2018 wanawake aslimia 45.3 tu walikuwa na kazi. 

Katika kipindi cha miaka 27 pengo la usawa wa kijinsia limepungua kwa asilimia mbili tu huku idadi ya wanawake na wanaume walioajiriwa imepungua duniani kote. 

ILO inasema licha ya kwamba kuna hatua zimepigwa tangu kupitishwa mkataba wa kwanza kuhusu wanawake kwenye ajira karne moja iliyopita, bado wanawake wanasalia kuwa wachache huku ripoti ikisema ni chini ya asilimia 26 ya uwezekano wa mwanamke kuajiriwa ikilinganishwa na wanaume.

Vikwazo vinavyokabili wanawake kwenye ajira

Elimu- Kiwango cha juu cha elimu inamaanisha uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ajira lakini wanawake hawapati mapato sawa na wanaume kwa viwango sawa vya elimu huku aslimia 41.5 ya wanawake wenye shahada ya kwanza hawajaajirwa ni asilimia 17 tu ya wanaume wenye elimu kiwango hicho.

Walezi- kitamaduni wanawake wanachukuliwa kama walezi na jamii na soko la ajira lina dhan hiyo na kwa sababu ya kazi zisizolipwa idadi kubwa ya wanawake hawako kwenye ajira ambapo wanawake milioni 647 ni walezi ikilinganishwa na milioni 41 ya wanaume.

Stadi kwa wakimbizi wa Syria ni muarobaini wa kuboresha maisha yao.
UNICEF/UN0201091/Herwig
Stadi kwa wakimbizi wa Syria ni muarobaini wa kuboresha maisha yao.

Wanawake walio na watoto katika nchi 51 asilimia 45.8 hawana ajira ikilimganishwa na asilimia 53.2 ya wanawake wasio na watoto wa umri huo.

Kwa mujibu wa ripoti changamoto zingine zinazoathiri usawa wa kijinsia ni malipo duni na utofauti wa malipo kwa misingi ya jinsia, ukatili na unyanyasaji katia maeneo ya kazi, sura mbali mbali za teknolojia ambazo zinatokana na mabailiko ya kidijitali zinazoathiri fursa na viwango vya kazi wanazozifanya wanawake na uwakislihi duni wa wanawake katika vyama vya kazi na wafanyakazi.

Mbinu za kufikia usawa wa kijinsia

Ili kuimarisha hali ya kazi kwa wanawake duniani ni muhimu kukabiliana na dhana zinazoshikiliwa kuhusu wanawake katika jami, na kwamba kazi yao ithaminiwe na vyeo vyao katika soko la ajira. 

Aidha ni muhimu kuwa nchi zitekelezeo makubaliano ya mkataba wa ILO kuhusu uswa wa kijinsia, kuzuia na kulinda dhidi ya ukatili na unyanyasaji katika sekta ya ajira, kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano ya malipo sawa kwa kazi sawa katika sheria na utekelezaji wake, kutoa vikwazo ikiwemo vya sheria vinavyowazuia wanawake kushiriki katika baadhi ya sekta na kazi, kuhakikisha likizo ya uzazi kwa mama baba kwa wote, kuwezesha mazingira sahihi ka ajili ya kupanda vyeo kwa wanawake.

Ripoti hii imetolewa kuelekea siku ya wanawake duniani machi 8 sambamba na ILO inapoelekea kutimiza miaka 100 tangu kuasisiwa mwaka 1919.