Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupunguza maambukizi ya VVU asilimia 30 ni habari njema:UNAIDS

Taswira ya seli zilizoambukizwa VVU (Rangi ya buluu na Kijani) zisizoambukizwa ni (rangi ya udongo na zambarau)
@Donald Bliss/NLM/NIH
Taswira ya seli zilizoambukizwa VVU (Rangi ya buluu na Kijani) zisizoambukizwa ni (rangi ya udongo na zambarau)

Kupunguza maambukizi ya VVU asilimia 30 ni habari njema:UNAIDS

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na maswala ya Ukimwi, UNAID leo limekaribisha matokeo yanayoonyesha kupungua kwa maambukizi ya HIV kwa asilimia 30 ambapo mbinu za kuzuia maambukizi ikiwemo, huduma ya kutoa maelezo na kupima VVU nyumbani ilitolewa ikiwemo kuwapeleka waliopatikana na HIV kwenye vituo vya tiba kwa kufuatana na muongozo wa nchi.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNAIDS iliyotolewa mjini Seattle, Marekani, utafiti huo ulifanyika kati ya mwaka 2013 na 2018 ukizilenga jamii 21 za mijini nchini Zambia na Afrika Kusini na kuwafikia watu milioni moja ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuwahi kufanyika.

UNAIDS kupitia mkurugenzi mkuu wake imepongeza timu ya watafiti walioshiriki akisema kuwa utafiti unaonyesha umuhimu wa judi za kuzuia, kupima na matibabu katika jamii akisema kuwa,  “nahimiza  wito wa UNAIDS wa wahudumu wa afya katika jamii barani Afrika, na umuhimu wa kuongezeka kwa uwekezaji katika kuzuia na kutibu HIV ikiwemo vifaa bora na mifumo ya kuwasilisha. Aidha imeonyesha umuhimu wa kuwafikia wanaume na vijana".

Kwa mujibu wa UNAIDS, utafiti ulikuwa na sura tatu ambapo upande mmoja ulihhusika na kuwasilisha mbinu za kuzia maambukizi ya HIV ikiwemo kutoa mafunzo na kupima, kuweka daraja ya wanoishi na HIV na vituo vya afya na kutembelea wanaoishi na HIV kuhakikisha wanafuatilia matibabu, kuchagiza wanaume kutairiwa kwa hiari kwa wale waliopatikana bila HIV, kuandikiwa kwa matibabu kuhusu magonjwa yanayoambukizwa kingono na huduma za kuzuia maambukizi ya HIV kutoka kwa mama hadi mtoto, ugawaji wa mipira kwa jamii na vipimo juu ya kifua kikuu.

Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI-ARV
Photo: Sean Kimmons/IRIN
Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI-ARV

Utafiti upande wa pili umeonyesha kuwa wanawake wa zaidi ya umri wa miaka 25 na wanaume zaidi ya miaka 40 ndio wanapata matibabu ya kupunguza makali ya HIV, ARVs tofauti na wanaume na vijana ambao wengi hawafikiwi na huduma.

UNAIDS inasisitiza kuwa hakuna mbinu moja pekee ya kuzuia VVU na kwamba ili kutokomeza Ukimwi, UNAIDS inapendekeza mambo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha kwamba watu wote wanoishi na VVU wanapata huduma ya ARVs , matumizi sahihi na endelevu ya mipira ya wanawake na wanume, kuwa na wapenzi wachache, na kutahiriwa kwa wanaume kwa hiari.

 Ripoti hiyo imetangazwa katika kongamano lililofanyika mjini Seattle Marekani linalohusu virusi vyenye tabia ya kujibadilisha ndani ya mwili ili kijifananisha na hali halisi ya mwilini ili viweze kuzaliana na kushambulia viungo vya asili kama seli.