Ofisi ya haki za binadamu Burundi yafungishwa virago baada ya miaka 23

5 Machi 2019

Kwa masikitiko makubwa Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet leo ametangaza kufungwa kwa ofisi ya haki za binadamu nchini Burundi.

Bi. Bachelet amesema ofisi yake imelazimika kuifunga ofisi ya Bunrundi rasmi Februari 28 mwaka huu kutokana na msisitizo wa serikali ya nchi hiyo “ni kwa masikitiko makubwa imetubidi kuifunga ofisi yetu nchini Burundi baada ya miaka 23 ya kuwemo nchini humo. Tangu ofisi ya haki za binadamu kuanzishwa nchini Burundi mwaka 1995 kwa miaka mingi tumesfanya kazi na serikali katika ujenzi wa amani, mabadiliko ya sekta ya usalama, mabadiliko ya sekta ya haki na kusaidia ujenzi wa taasisi na uwezeshaji wa jamii katika masuala ya haki za binadamu.”

Kufunguliwa kwa ofisi ya haki za binadamu Burundi

Ameongeza kuwa ofisi ya haki za binadamu nchini Burundi ilianzishwa mwaka 1995 kufuatia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliotendeka kufuatia mauaji ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Melchior Ndadaye.

Ofisi ya haki za binadamu ilisaidia kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinajumuishwa katika utekelezaji wa mkataba wa Arusha ambao ndio ulikuwa uti wa mgongo wa utulivu wa nchi hiyo kwa miaka mingi.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa pia ilikuwa na jukumu kubwa katika kuanzishwa kwa tume huru ya kitaifa ya haki za binadamu, tume ya ukweli na upatanishi, mabadiliko ya sharia na kufufufuliwa kwa taasisi na mashirika imara ya asasi za kijamii.

Dosari katika haki za binadamu Burundi

Kwa bahati mbaya , Kamsihina mkuu wa ahki za binadamu zmesema mafanikio yote yaloiyopatikana katika haki za binadamu yakaanza kuingia dosari mwaka 2015.

Oktoba mwaka 2016 serikali ya Burundi iliamua kusitisha ushirikiano wowote nan a ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi kwa sababu ya ripoti iliyotolewa na tume huru ya uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za binadamu ilkiyoanzishwa na Baraza la Haki za .

Doudou Diene, Rais wa tume ya uchunguzi kuhusu Burundi.
ONU Info/Florence Westergard
Doudou Diene, Rais wa tume ya uchunguzi kuhusu Burundi.

 

“Hii inamaanisha wafanyakazi wetu wa haki za binadamu walipokonywa uwezo wa kuchunguza kwa kina madai ya ukoiukwaji wa haki za binadamu licha ya hatua hiyo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva nay a Burundi zimeendelea kupokea madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili.“

Miaka miwili baada ya kusitisha ushirikiano , mnamo Disemba 5 mwaka 2018 , serikali ya Burundi iliomba kufungwa kwa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi ikitoa maelezo kwamba serikali imepiga hatua kubwa nay a kutosha ya kuweka mfumo wa kulinda haki za binadamu hivyo uwepo wa ofisi ya Umoja wa Mataifa hauna sababu tena.

Utendaji wa OHCHR kuhusu haki za binadamu Burundi

Bi Bachelet amesema “Ripoti zetu kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Burundi daima imekuwa ni katika nia Njema ya inayolenga kusaidia kuchagiza na kulinda haki za binadamu nchini humo. Lakini nimevunjwa moyo na hatua ya Burundi kutotoa ushirikiano katika miaka ya karibuni hasa kwa mfumo wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu , ambapo serikali ilienda mbali Zaidi hata kutishia kuwashitaki wajumbe wa tume huru ya kimataifa ya uchunguzi iliyoanzishwa na Baraza la haki za binadamu “

Bachelet amewashukuru watetezi wengi wa haki za binadamu na asasi za kiraia nchini Burundi ambao wamefanya kazi kwa kujitolea kwa moyo wote , bila kukata tamaa, kwa ujasiri na utaalam katika migogoro mingi ya kisiasa na kijamii nchini humo ingawa pia kwa masikitiko amesema wengi wa watetezi haoo hivi sasa wako rumande au wamelazimika kwenda ukimbizini.

Nini kitafuata

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kutoboka kwa sufuria sio mwisho wa mapishi kwani “Hata kama ofisi zetu zimefunga mlango Burundi tutaendelea kutafuta mbinu zingine za kufanya ili kuhakikisha tunaeleza yanayojiri na kutia hofu katika haki za binadamu  na kusaidia katika kuelimisha, kuchagiza na kulinda haki za binadamu nchini humo” amesema Michelle Bachelet.

Ameongeza kuwa serikali ya Burundi imeelezea msimamo wake wa kufanya kazi na ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa baada ya kufunga ofisi yetu nchini humo , na tuko tayari kushirikiana vilivyo. Pia natoa wito kwa serikali ya Burundi kushirikiana na mifumo yote husika na masualka ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikiwemo wataalam huru na vyombo vya mikataba ya haki za binadamu.

 

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter