Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watakaoingia kinyan’ganyiro cha kumrithi Graziano da silva FAO watajwa

Mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva.
FAO/Giuseppe Carotenuto
Mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva.

Watakaoingia kinyan’ganyiro cha kumrithi Graziano da silva FAO watajwa

Masuala ya UM

Wagombea wataokaojitosa kwenye kinyan’ganyiro cha kumrithi Jose Graziano da Silva kama mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, wametajwa hii leo na shirika hilo.

Wagombea hao watano wamewasilishwa kwa FAO na nchi wanachama na watapigiwa kura Juni 2019 ili apatikane mmoja atakayekuwa mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo.

Uchaguzi wa kumpata mkurugenzi huyo mpya atakahudumu kwa awamu ya miaka minne kuanzia Agosti 2019 utafanyika kwenye kikao cha 41 cha cha ngazi ya juu cha  FAO kinachoanza mjini Roma Italia 22-29 Juni.

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha majina ya wagombea ilikuwa Februari 28 mwaka huu.

Wagombea wa kiti cha ukurugenzi FAO

Majina ya wagombewa hao watano ambao kila mmoja aliteuliwa n anchi yake ni Médi Moungui (Cameroon), Qu Dongyu (China), Catherine Geslain-Lanéelle (France), Davit Kirvalidze (Georgia) na Ramesh Chand (India).

Nchi wanachama watapiga kura ya siri kwa mfumo wa “nchi moja -kura moja”uchaguzi utakaohitaji mgombea kupata idadi ya kura nyingi kuhalalishwa.

Mkurugenzi mkuu ajaye wa FAO atashika hatamu kuanzia Agosti Mosi 2019 hadi 31 Jualai 2023 na ataweza kuteuliwa tena kwa muhula mwingine mmoja wa miaka 4. Mkurugenzi huyo mpya atamrithi Jose Graziano da Silva aliyechaguliwa mwaka 2011 na kuhudumu mihula miwili ya miaka minne minne. Tangu kuanzishwa kwa shirika la FAo mwaka 1945 kumekuwa na wakurugenzi wakuu 8 wa shirika hilo ambao ni Sir John Boyd Orr, kutoka Uingereza, 1945-1948, Norris E. Dodd, kutoka Marekani ,1948-1954, Philip Vincent Cardon, United States, 1954-1956, Binay Ranjan Sen, kutoka India, 1956-1967,  Addeke Hendrik Boerma, kutoka Uholanzi, 1968-1975,  Edouard Saouma, kutoka Lebanon, 1976-1993 , Jacques Diouf, kutoka Senegal, 1994-2011 , na José Graziano da Silva,kutoka  Brazil, 2011-2019 .