Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Venezuela ihakikishe uwepo wa haki pasina upendeleo-Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa.

Bendera ya jamhuri ya Venezuela (katikati) ikipepea katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.
UN /Loey Felipe
Bendera ya jamhuri ya Venezuela (katikati) ikipepea katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

Venezuela ihakikishe uwepo wa haki pasina upendeleo-Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa.

Haki za binadamu

Diego García-Sayán, ambaye ni mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na wanasheria, ametoa wito kwa mamalaka nchini Venezuela kuchukua hatua za kuhakikisha kunakuwa na uhuru wa mahakama.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na ofisi  ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi, mtaalamu huyo amesema, “taasisi zote za Venezuela zinatakiwa kuheshimu, kukuza na kuhakikisha uhuru wa mahakama usio na upendeleo, wakiwemo majaji na waendesha mashitaka ili waweze kuwa na huru katika mazingira ya shinikizo. Ni muhimu kuwa katiba na mikataba ya haki za binadamu viheashimike.”

Aidha Bwana García-Sayán ameeleza kusikitishwa kwake na hali ya shinikizo kuwekwa katika mfumo wa mahakama ili watende kinyume visivyo dhidi ya upinzani ambao unaongozwa na Juan Guaidó ambaye alitangazwa na Bunge kuwa rais wa mpito.

“Hatua zinazochukuliwa dhidi ya Guaidó na shinikizo dhidi yake havikubaliki. Ninalaani uchunguzi wa jinai unaofanyika kwasababu unaweza kuwa ni kwasababu za kisiasa. Matamko ambayo yametolewa na Tarek William Saab ambaye ni muungaji mkono wa Rais Maduro kuhusu uchunguzi dhidi ya  Guaidó tayari yanaweza kuwa yameathiri imani ya kisheria,” amesisitiza Bwana García-Sayán.

Mtaalamu huyo aambaye tayari ameshawasilisha mawazo yake kwa serikali ya Venezuela, amesisitiza zaidi kwa kusema kuwa Venezuela inatakiwa kupanga vyombo vya serikali katika namna ambayo inaendana na taratibu za kimataifa za kuhakikisha utawala wa kisheria, uhuru na kutokuwa na upande katika maamuzi ya mahakama na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.