Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna kinachohalalisha utumiaji wa risaasi za moto dhidi ya waandamanaji Gaza:UN

Baraza lataka uchunguzi kuhusu kilichotokea Gaza
Picha ya OCHA oPt
Baraza lataka uchunguzi kuhusu kilichotokea Gaza

Hakuna kinachohalalisha utumiaji wa risaasi za moto dhidi ya waandamanaji Gaza:UN

Amani na Usalama

Tume huru ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi kuhusu maandamano kwenye eneo linalokaliwa la Palestina leo imewasilisha ripoti yake kjwenye Baraza la haki za binadamu iliyobaini ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu kwenye ukanda wa Gaza. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo uchunguzi ulijikita kwenye maandamano yaliyofanyika Ukanda wa Gaza yakijulikana kama “maandamano makubwa ya marejeo na kumaliza hali ya kuzingirwa”.Akizungumzia matokeo ya uchunguzi wao mwenyekiti wa tume hiyo Santiago Canton kutoka aArgentina amesemasa

Tume imebaini kuna sababu nzuri za kuamini kwamba, askari wa Israeli walifanya ukiukwaji mkubwa wa haki za kimataifa za binadamu na sheria za kibinadamu. Kwa hakika ukiukwaji huu unahitaji uchunguzi wa uhalifu na kuchukuliwa sheria, tunaitolea wito Israel kuendesha uchunguzi wa kina dhidi ya uhalifu huu mkubwa na kutoa haki kwa waliouawa na kujeruhiwa.”

Pia ameongeza kuwa baadhi ya ukiukwaji huo unaweza kuwani  uhalifu wa vita au uhalifu dhidi ya ubinadamu, na lazima uchunguzi wake ufanyike mara moja.

Tume hiyo ilipewa jukumu na Baraza la Haki za binadamu mwezi Mei 2018 kuchunguza madai yote ya ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili unaokiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu katika eneo la Palestina linalokaliwa wakati wa maandamano makubwa yaliyoanza Gaza tarehe 30 Machi 2018  hadi tarehe 31 Disemba 2018.

Watoto ni waathirika wa mashambulizi kama hapa shule ya wasichana iliyosambaratishwa kwa mabomu huko Shuja'iyeh, mashariki mwa mji wa Gaza.
UNICEF/Eyad El Baba
Watoto ni waathirika wa mashambulizi kama hapa shule ya wasichana iliyosambaratishwa kwa mabomu huko Shuja'iyeh, mashariki mwa mji wa Gaza.

Katika kipindi hicho waandamanaji 600 walipigwa risasi na wanajeshi wa Israel na Wapalestina 189 waliuawa wakati huo 183 kwa kutumia risasi za moto, na 35 kati ya waliouawa walikuwa ni watoto, wahudumu wa afya watatu na waandishi wa habari wawili.

Ripoti imeendelea kusema kuwa wapalestina zaidi ya 6000 walijeruhiwa pia askari wanne wa Israel walijeruhiwa na mmoja kuuawa. Akifafanua kuhusu ukiukwaji huo mjumbe wa tume Sara Hossain amesema “hjkuna kinachohalalisha mauaji na kujeruhi waandishi wa habari, wahudumu wa afya na watu ambao hawatoi tishio lolote .

Akijibu hoja ya madai kwamba wandamanaji hao walikuwa wakifanya ghasia Sara amesema

“Asilimia kubwa ya waandamanaji hawakujihusisha na aina yoyote ya ghasia , kulikuwepo wanawake na watoto, kulikuwepo watu waliokuwa wakisoma mashairi, wakipiga muziki, wakipeperusha bendera vitu ambavyo kwa njia yoyote ile haviwezi kuchukuliwa kama ni ghasia nadhani suala la kuwachukulia kwamba waandamanaji wote walikuwa wanafanya ghasia hatukubaliani nalo.”

Lakini pia tume imesema imebaini kwamba baadhi ya wajumbe wa kamati ya kitaifa waliandaa maandamano ambao wanajumuisha wawakilishi wa Hamas na waliwachagiza au kuwatetea waandamanaji waliofama mashambulizi kwa kutumia vishada na Maputo na kusababisha hofu miongoni mwa raia na pia uharibifu wa vitu Kusini mwa Israel hivyo tume ikahitimisha kwamba uongozi wa Hamas Gaza ulishindwa kuzuia vitendo hivyo.

Tume ilifanya mahojiano na watu 325 wakijumuisha waathirika, mashuhuda na wahusika na kukusanya nyaraka zaidi ya 8000, na sehemu kubwa ya uchunguzi ilijumuisha mitandao ya kijamii, sauti na video za matukio ikiwemo picha zilizorekodiwa na ndege zisizo na rubani au drone , kwa mujibu wa Betty Mirungi mmoja wa wajumbe wa tume hiyo tayari mahakama ya kimataifa ya uhalifu inatiwa hifu na hali hiyo ya Gaza.