Mamilioni wanufaika na muamko wa kutokomeza kutokuwa na utaifa Afrika Magharibi-UNHCR

27 Februari 2019

Mamilioni ya watu wamekwepa kutokuwa na utaifa Afrika Magharibi kufuatia mataifa mengi kudhamiria kuhakikisha kuwa kila mtu anapata utaifa ifikapo mwaka 2024 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Kupitia taarifa yake UNHCR, inasema watu 37,250 ambao walikuwa hatarini kukosa utaifa, walipokea vyeti vya kuzaliwa nchini Burkina Faso mwaka jana.

Nchini Gunea-Bissau, wakimbizi 7,000 wengi wakiwa waliokimbia nchini humo bila vitambulisho wanapatiwa uraia.

UNHCR imeongeza kuwa mamilioni ya watu wamenufaika Niger, kufuatia usajili wa vyeti vya kuzaliwa na usajili wa ndoa kufuatia mpango wa kutoa huduma hizo bila malipo katika azma ya kutokomeza hali ya kutokuwa na utaifa ya jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS.

UNHCR katika taarifa yake imesema usajili wa ndoa na kuzaliwa ni muhimu katika kutoa ulinzi na kuhakikisha kwamba raia wanapa huduma ya elimu, afya na ajira, haki ambazo wengi hawatili maanani.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter